“Ulizia pesa wakuzime kama taa”- Joh Makini

Joh_Makini1_lrg

“Ulizia pesa wakuzime kama taa”- Joh Makini

Muziki wa kizazi kipya yan Bongo Fleva/Hiphop umeendelea kukua siku baada ya siku.

Inafurahisha kuona ni jinsi gani wasanii wamekuwa wakionyesha uwezo wao katika ramani ya muziki wa afrika sasa. Ingawa mafanikio walinayo ni tofauti kabisa na majina yao.

Binafsi sifurahishwi na mwenendo huu wa kuwa na masikini wenye majina makubwa.

Katika wimbo wa Sanaa wa Lord Eyez aliyomshirikisha Joh Makini walijaribu kusema mengi yenye tija kama swala la kusema “Sanaa isiwe ngazi yakutengeneza masikini wenye majina makubwa, sanaa iwe ni kazi”

Lakini katika wimbo wa Stimu zimelipiwa wa Joh Makini amesema “Ulizia pesa wakuzime kama taa, ni somo rahisi lisilohitaji hata tution”

Maneno hayo yanaendana kabisa na uhalisia wa sasa kwenye maisha ya muziki wa bongo fleva/hiphop. Ni wazi wengi hufanya matamasha ya bure na matamasha hayo humnufaisha mdau pekee, na kama ukionekana umeulizia malipo basi swala la wewe kupotezwa kimuziki ndilo ambalo hufuata.

Katika wimbo wa Bizness wa Izzo Bizness akiwa na Suma Lee yeye amesema “Wanaonyesha zote dalili show zao wanafanya bure tuko sawa hatuchekani”

Kauli zote mbili ziko katika mzunguko wa Sanaa ya muziki kwa ujumla. Leo tumeona hata baadhi ya wachambuzi wa maswala ya muziki wakijaribu kuwatia hofu wasanii juu ya kupotea endapo tu watahoji juu ya malipo yao. Hili ni jambo la kushangaza kuona wachambuzi wakiwa mstari wa mbele katika kuendeleza hofu juu ya wasanii. ‘Ujinga’

Katika uhalisia muda umefika wa wasanii kuamka vyema wajue thamani walinayo, kazi wanayofanya ni kubwa mno. Unajua kufanya mtu acheze au aimbe muziki wako si jambo ndogo.

Hivyo huu ni muda muafaka wa kuamka na kutambua thamani ya muziki wako, miaka ya sasa ni ngumu mtu mmoja kuwa roho ya muziki wote. Ni muda wa kuulizia malipo kabla ya kusaini mikataba hewa.

Muda ndio huu amka msanii, hakuna wa kukuzima kama taa

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez