TUSUBIRI KETE ZAO ZA TATU ILI WADHIHILISHE UKALI WAO!

SennMicrophone

Hakuna mpenzi ,mdau,mfatiliaji au shabiki wa mziki ambae hafarijiki kama sio kufurahi kabisa na hatua tuliyopiga katika mziki wetu ndani na nje ya nchi ama hakika ni jambo kubwa sana ambalo linatutangaza vyema duniani kote ukiachilia mbali mpira,ubunifu na siasa.

Ni ukweli usiofichika kuwa tunawasanii wengi sana ambao wameshatoka na wengine bado wanaendelea na harakati za kuhakikisha kuwa nao wanapata nafasi ya kusikika na kuweza kukamilisha ndoto zao.

Billnass na Chemical ndio wasanii ndio wasanii ninao subiria kete zao za tatu ili wadhihilishe rasmi kuwa nao ni miongoni mwa wasanii wakali ambao wana wigo mkubwa wa mashabiki licha ya kuwa na muda mchache katika game ya mziki huu wa kizazi kipya.

BILLNASS

Bill Nass FT Naziz

Ni msanii ambaye ameshtua mashabiki wengi sana na hata kwa wasanii wenzake ambao wapo kwenye game mda mrefu alianza vema kwa trak yake ya kwanza kusikika radioni alio washirikisha Nazizi pamoja TID katika wimbo uitwao RAHA huu wimbo uliweza kumfikisha mbali sana billnass kwa kushika nafasi za juu katika chat mbali mbali za mziki na kukaa kwa muda mrefu kama tunavyojua mziki unavitu vingi sana ambavyo huwa vinaweza kumpandisha msanii au kumshusha na kumpoteza kabisa kwake billnass alijikuta akiingia katika beef ndogo na msanii NeyWamitego baada ya kusema kuwa billnass hakupaswa kuingia katika tuzo za kilimanjaro music award katika kipengele cha msanii anaechipukia.

Billnass hakuishia hapo kwani mwaka huu umekua mzuri zaidi kwake baada ya kutoa wimbo wa Ligi ndogo alioshirikiana TID   ambao unaendelea kufanya vizuri mpaka sasa Katika vituo vya radio na chat mbalimbali za mziki hapa nchini ligi ndogo imeongeza imani kubwa kwa mashabiki wa billnass.

CHEMICAL

CHEMICAL
Hakuna asiejua uwezo,style na flow za huyu rapper wakike mwenye nyimbo mbili tu mpaka sasa nakufanikiwa kuongeza idadi ya marapper wa kike wanao fanya game ya hip hop Tanzania wengi tunajua wasanii huwa wanaanza na kazi nzuri ya kwanza na wakashindwa kufanya vizuri katika kazi zitakazofata kwa Chemical haijawa hivyo na kafanikiwa kuondoa hofu kubwa mashabiki wake toka alipaachia Sielewi na kuja na mkwaju wa pili VIP  chemical amezidi kuwa mkubwa japo siamini kama VIP ni diss trak kwa rapper mwenzake Stosh.

Billnass na Chemical ni wasanii wanaoendana kwa jinsi walivyo ingia kwenye game na wote kuwa na nyimbo mbili kila mmoja ambazo zinafanya vizuri.Ngoja tuwasubiri katika ujio wao mpya ambao tunategemea makubwa zaidi kutoka kwao.

Imeandikwa na JOHN SIMWANZA TSJ.

Powered by Tizneez.com

twitter@tizneez

intagram@tizneez

facebook@tizneez