Tumia akili kwenye mchanganuo wa hoja- Baba Levo

Baba-Levo

Tumia akili kwenye mchanganuo wa hoja- Baba Levo

Mwenye hekima daima huchunga kinywa chake katika kila neno atakalo kuwa anasema, haijalishi ni eneo gani bali katika maisha yake ya kila siku.

Katika ramani ya muziki wa kizazi kipya kumekuwa na jambo la kustua wengi hasa baada ya Ruby kusema hakuweza kupanda kwenye jukwaa la Fiesta Mwanza maana hakuna maslahi kwa upande wake.

Hoja hii kila mtu ameipokea kwa namna yake, ila ni hoja ambayo haitaki majibu kutoka kwa mtu mwingine zaidi ya kamati ya Fiesta na Ruby mwenyewe. Wengine wote hatujui ukweli umesimama wapi kati ya hawa wawili, maana hakuna aliyeona mkataba wao kipindi wanasaini, ndio maana Team Tizneez tuliweka mahojiano yake kama yalivyo.

Kutumia akili katika kuchambua hoja kunahitaji akili ya ziada sio kukurupuka mbele ya jamii.

Baba Levo ambaye ni diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini Mkoani Kigoma, kupitia mtandao wa picha “Instagram” aliweka picha ya Ruby na kuandika maneno yanayosomeka “Hii kick anayotengeneza ruby ya kuwadiss CLOUDS ni yakujipakaa #MAVI Mziki unahitaji uvumilivu sana.. Angetulia akomae kwanza #D_ONE

Sifa ya kiongozi ni kuwa na busara hata kuweka hoja zenye maana ambazo zitajenga. Baba Levo ametoa hoja dhaifu maana ni wazi amegeuka kuwa mtabiri na imeonyesha ni kiasi gani hakutumia akili katika mchanganuo wa hoja hii.

Baba Levo hakusita kuandika tena “Kumfananisha Ruby na Lady Jaydee ni utoto, Jide alisubiri akomae kisha akazingua akiwa na pesa haka hata geto hakajajipanga eti kanazingua haya tutaona”

Mimi nimefanya mohojiano na Ruby na alisimamia swala moja tu la maslahi, kudai maslahi yake si sababu ya Lady Jaydee bali ni yeye na nafsi yake.

Kama Diwani huyu anasema Ruby angesubiri mpaka apate hela ndio azingue, ina maana hata yeye akipata pesa atazingua juu ya maslahi yake.  Lakini kwa kumsaidi Baba Levo swala la kudai maslahi si mpaka upate hela isipokuwa maslahi unaweza kuyadai muda wowote bila kujali una nafasi gani bali haki yako iko wapi kwa wakati huo.

Hivi hizi ni kauli za diwani ambaye anaongoza watu kwenye kata yake, siachi kujiuliza anaongoza watu wa aina gani? Pia Baba Levo akumbuke miaka hii si miaka ya zamani, vijana wameamka na wanajua haki za kwa 100%. Pia inaonyesha ni jinsi gani Baba Levo alivyo na kiwango kidogo cha mawazo bali mtu mwenye sifa mbele ya jamii.

Ni vyema akamwacha Ruby afanye kile ambacho kwake anaona sahihi na sio kumuingilia na kuleta mitazamo dhaifu mbele ya jamii.

 

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez