’Tujifunze kufikiria kesho zetu’ Harmonize

’Tujifunze kufikiria kesho zetu’ Harmonize

Kumekuwepo na maneno mengi katika mitandao ya kijamii juu ya msanii mchanga Harmonize kuhusu mahusiano yake na msanii bongo muvi ambaye ni maarufu kwa jina la Wolper.

Ni muda mrefu wengi wamekuwa wakiandika na kuposti kuwa wameachana na hawako pamoja.

Ambapo leo Harmonize amethibitisha kuwa ameachana rasmi na Wolper. Harmonize amesema “Kusema ukweli nilikuwa na mipango mingi na Wolper nyumbani nikampeleka lakini kila mwanadamu ana nyongo kwasasa sipo naye tena”

Jambo la kuachana katika mahusiano ni jambo la kawaida kabisa, na lipo kwenye maisha ya kila mtu na hutokea kila siku.

Hainishangazi juu ya Harmonize kuachana na Wolper na kuzungumziwa Zaidi katika mitandao ya kijamii. Ukitazama kwa umakini ni wazi alitaka mno kuzungumziwa tangu kuanza kwa mahusiano  yao mpaka mwisho wao.

Kuanza kwa penzi lao kulikuwa na kila aina ya mbwembwe, uchafu, ulimbukeni na mengine mengi ambayo yalikuwa ni chukizo juu ya watu makini ambao huwa hawako tayari kutazama mengi yaliyojaa upuuzi yasiyo na faida katika kazi zake za muziki Harmonize.(Kiki)

Katika mahojiano mengi aliyokuwa akifanya Harmonize alikuwa haachi kuzungumzia mpenzi wake huyo wa zamani Wolper, na hata kutetea yaliyomengi mabaya yale ya kufanya mambo ya chumbani hadharani tena bila aibu.

Lakini wakati huo alisahau maisha ya nje ya muziki wake, wasanii wengi akiwemo Harmonize husahau kuwa kuna maisha nje ya muziki. Na sio kila jambo ni lazima ulionyeshe katika ulimwengu wa mashabiki wako wa muziki.

Leo baada ya kusema ameachana na Wolper tegemea kuona zile video zake alizokuwa anafanya mambo ya aibu zikisambaa Zaidi katika mitandao ya kijamii, maana zipo kurasa nyingi zisizojali kuhusu utu wa mtu.

Na katika uhalisia video hizo ni wazi zitakuwa chukizo Zaidi kwa Wolper kulingana na kasumba tuliyonayo watanzania wengi.

Ni wazi watu wote maarufu wanapaswa kujifunza kuwa sio kila jambo uliweke hadharani, maisha nje ya umaarufu yapo na yanapaswa kuishi kama yalivyo.

Pia ni wazi msanii Harmonize hakupaswa kueleza mengi juu ya kuachana na Wolper, kusema tu tumeachana ingetosha. Maana katika uhalisia haina faida yoyote kwa mashabiki wake, ila “Mchuma janga hula na nduguze”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment