Truebadour Wasanii wengi wa hiphop bongo wana uelewa finyu.

photo

Truebadour Wasanii wengi wa hiphop bongo wana uelewa finyu.

Trubadour ni moja ya wasanii wa hiphop wanawakilisha vyema katika mitaa mingi yenye vijiwe vya hiphop.

Akiongea na Team tizneez kuhusu lawama nyingi ambazo wasanii wengi wamezitoa kutoka kwenye wimbo wake wa kwa Hewa alisema “

“Ni kweli Baada ya kutoa wimbo wangu wa Mpya wa HEWA. Kumekua na maneno ya mitandaoni kwa wasanii wanaohisi kuzungumziwa. Nilichogundua ni kua wasanii wengi wa hip hop bongo wana uelewa finyu kuhusu lugha ya ufananishi. Kwasababu kila nilichoongea kina maana zaidi ya moja. Vitu ninavyoweza kuweka sawa ni kuwa nimemzungumzia ROMA kama msanii na kama Mji uliopo Italia. ROMA msanii ni Hewa kwa sababu ni msanii mwenye ujumbe wa wa uongo. Kwa mfano amewahi kusema ”pesa kweli mwanaharamu ilimponza mpaka Petro” ukweli ni kwamba pesa haijawahi kumponza Petro bali Yuda. Pili amewahi sema ”nasimama kama kanisa la KkT” hakuna kanisa la KkT bali KkkT kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania. Simply Roma ana uwezo mdogo. Msanii kama Bagdady kwanza haeleweki anachofanya na yupo mbelembele kwa kila kitu ndo maana ya HEWA kwake. So anatakiwa kuwa compitent kwenye vitu anavyofanya. NAY WA MITEGO kisanaa simjui.  Giggy Money anafanya mchezo na ajira za watu so akiendelea wengine tutaacha ndo maana katajwa. Wengine wote wanaohisi kutajwa wasikilize vizuri watagundua kila kilichosemwa ni lugha ya picha kina maana nyingine.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez