Tanzia! Msanii Sam wa ukweli afariki Dunia.

Tanzia! Msanii Sam wa ukweli afariki Dunia.

Sina raha na kwetu wapo ni moja ya nyimbo zake ambazo zilimuweka juu kwenye uwanja wa muziki.

Sam ni moja ya wasanii ambao walikuwa na upekee wa sauti yake kulinganisha na wengine.

Mauti yamemkuta katika hospitali ya Palestina Sinza mapema usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Na mwili wa marehemu umeifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala huku taratibu za mazishi zikiendelea kufanyika.

Yapasa tusifadhaike kwa maana “Chenye asili ya kiumbe hakikosi deni la kifo” kwa nyakati zake ametimiza.

Team Tizneez tunatoa pole kwa ndugu, jamaa, na marafiki walioguswa na msiba huu.

Na twakutakia pumziko jema katika maisha ya kifo ndugu yetu Sam wa Ukweli. Naam! Mtu atapita isipokuwa muziki”

#TuzungumzeMuziki