Tanzania Day yaingia dosari, Hivi Zavara unadhani sisi bado washamba kama enzi zenu? Nikki Mbishi ahoji.

Tanzania Day yaingia dosari, Hivi Zavara unadhani sisi bado washamba kama enzi zenu? Nikki Mbishi ahoji.

Nikki Mbishi ni msanii wa hiphop ambaye mara zote amekuwa ni mwepesi mno kuweka uwazi kile ambacho yeye anakiamini.

Mapema leo hakusita kutuma waraka wake kwa Team Tizneez ili tuweze kuwafikishia watanzania.

Ambapo Nikki Mbishi ni moja kati ya wasanii wanne walioshiriki katika wimbo wa Tanzania Day, akiwemo Wakazi, Songa na P The Mc.

Katika waraka wake huo Nikki Mbishi ameandika

“Hivi ni mpaka lini watanzania walio nje (Baadhi) wataelendea kutufanya sisi(Wasanii) wa Tanzania mafala?

Ina maana mpaka leo hawajaona utandawazi ambao uko dhahiri kabisa na asilimia kubwa umewafikia hususan tulio mazingira yenye ukubwa wa teknolojia kwa udogo wake?

Kwanini wachumia tumbo wanapenda kujisitiri kwenye kivuli cha udhati wa harakati na kujifanya wana mapinduzi au mageuzi ili hali wao ndio wenye kunufaika kuliko wale wanao waunga mkono?

Mambo mengi yameishia njiani kwa ajili ya watu kama hawa ambao ni Mungu tu ndio mwenye dhamana ya uhai wao kwa sababu sio rahisi kudhani watu wote wana ujinga wa kiwango sawa.

Huu sio muda wa kuagizwa ng’ombe 10 halafu ukaleta magumashi ya kupeleka mbuzi 20 ukadhani umefidia au kuziba pengo kana kwamba hutodaiwa gharama zilizopotea kisa umeleta mbuzi 20.

Unadhani hatujui kuwa thamani ya mbuzi 20 haifikii thamani ya ng’ombe 10?

Tulikuwa na mambo mengi sana ambayo yaliuliwa na hawa hawa jamaa wanaojifanya wanajali huu utamaduni wetu wa Hip Hop mfano:Words And PIctures (WAPI),B-Connected,Tuzo,Matamasha mengine mengi tu.
Hawa jamaa zetu hupata nafasi ya kuwa sehemu ya viunganishi vya masuala mengi ya kisanaa wakiwa nje ila ubaya wanajivika umeneja na “UMIDDLE MAN” wapige kata funua halafu walengwa mbaki na majonzi kama si maumivu.

Ni hivi waliotufuata kutuambia suala la TANZANIA DAY 2018 (Marekani) ndio wale wale waliotuliza mara zote miaka iliyopita,tumefanya vitu kwa heshima yao kwetu wala si kwa kuwaamini maana tunajua nao ni waganga njaa kama sisi,tumewaza labda baadha ya miaka dhahari watakuwa wamebadilika kumbe bado wako vile vile.

Hivi wewe ZAVARA unadhani sisi bado wajinga na washamba kama enzi zenu kwamba hatujui kitu mpaka leo?

Mbona mnapenda kujifanya mna shida kuliko sisi ili hali unaijua sanaa ya Bongo na maisha ya wasanii jinsi tunavyopigana vikumbo kutafuta mkate wa kila siku,bora wewe hata huna hela walau unaishi kwenye joto lenye baridi ukilinganisha na sisi tulio kwenye joto lenye joto.

Mauzo ya Album yangu ya kwanza #SautiYaJogoo kwa upande wa online yaliratibiwa na mtanzania pia ambaye yupo huko ambapo licha ya album hiyo kuwa na nyimbo zilizofanya vizuri zaidi kama Punchlines,Kila siku,Play Boy,Jogoo,Nyakati za mashaka,Au n.k ambazo ndizo ziliniweka kwenye ramani ya muziki wa Tz,naomba niseme hiyo ndiyo album niliyokula hasara kuliko kawaida hata sijajua mpaka leo share yangu iko wapi,sawa wakate wanachokata ila mbona hamjawahi kunitumia hata dola 100 za online sales naongelea iTune na Cdbaby ambapo album inapatikana?Hapo bwana Steve Nyabero alinipanga mpaka akaanza kuniambia nimpe CV anitafutie ajira ofisini wakati tayari nishajiajiri.
Haikunikatisha tamaa nikaendelea na kutoa albums kivyangu licha ya kutoambulia hata punje ya mchele kwenye mpunga uliovunwa.

ZAVARA,acha ujanja ujanja wa Temeke huo ndio unaofanya hata u-legend wako kuwa wa kidwanzi, jifunze kula na vipofu sio nyama na matonge makubwa yote ule wewe halafu sisi utupange, tushakuwa watu wazima, tulikutana sina hata majukumu ila sasa hivi nina watoto wawili wakubwa(Malcolm na Nathan) muda mwingine unaweza hata kupelekwa kwa Makonda sababu unakwama kuprovide kwa familia ipasavyo na watu wakadhani unapenda kumbe wadwanzi ambao watoto wao wana insurances za maisha ndio wanatudhulumu ili tuendelee na hii demokrasia ya manyani.

Nimechoka #KLMY nitasema popote nitakapo simama, sitaki ushoga na mbugila yeyote mwenye nafsi ya upigaji au dhuluma.

Lipeni watu stahiki zao,by the way HAKUNA TENA CHA TANZANIA DAY 2018(Dallas,Texas) wala Tandale,weka mpunga tuchekeche sio blah blah na kupotezeana muda, halafu kama ipo ipo tu.

Heshima yangu imeishia hapa naongea na wote mliosababisha disappointments kwa makusudi mkiongozwa na CHIEF RHYMESON wa zamani ambaye ni ZAVARA wa siku hizi.

Wenu mtiifu nisiyekula wala kulala kwenu,
Nicas J.Marwa Machuche alias Nikki Mbishi(UNJU)
2018.