Takwimu za msanii toka Tamaduni Muzik zazima kauli ya Mr blue

index

Takwimu za msanii toka Tamaduni Muzik zazima kauli ya Mr blue

Azma Mponda ni msanii tokea Tamudini muziki ambaye sio msanii ambaye amekuwa akizungumziwa kwenye vyombo vya habari kama ilivyo kwa wengine.

Siku 4 nyuma kupitia mtandao wa picha “Instagram” Mr Blue aliandika “Nyimbo yangu ya mboga saba imekuwa nyimbo ya kwanza ya Rap/Hiphop kutimiza 1 milioni ndani ya miaka hii miwili.Achana na hizi za kuimba nazungumzia hiphop, kama una wasiwasi na hilo hakikisha harafu mtag aliyewahi kufikisha idadi hiyo.Asante mungu asanteni wadau”

Lakini baada ya muda mfupi kupitia kwa wadau wa muziki wa hiphop na baadhi ya wasanii walioneka kupinga kauli.

Ambapo hawakusita kushare picha ya video ya Azma Mponda inayoitwa Jinsi ya kumfikisha mpenzi wako, ambayo iliweza kufikisha views hao ambao Mr Blue alisema hakuna msanii wa hiphop ambaye ameweza katika miaka hii miwili.

Hivyo Azma anasimama kama namba moja katika hilo swala kwa mujibu wa wadau wa hiphop na baadhi ya wasanii.

Licha ya kuwepo kwa hoja toka kwa mashabiki wa hiphop kusema Mr Blue sio msanii wa hiphop.

Je wewe una maoni gani kwenye hili? Mr Blue ni msanii wa hiphop au sio?

Tupe comment hapa chini.

Picha chini juu ya video hizo mbili.

Capture

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez