Taarifa muhimu kutoka kwa Baghdad

Capture

Taarifa muhimu kutoka kwa Baghdad

Tar 31 july ninatarajia kuzindua video ya wimbo wangu wa FOLENI ambao nimemshirikisha Isam Muandaaji wa kazi zangu nyingi kama Una akili wewe niliomshirikisha ROMA Ninae niliomshirikisha NANDy na nyingine nyingi. Wimbo huo ambao umefayika katika studio za M.I.L zilizoko sinza kwa remy ilitoka rasmi tar 25 june hivyo itakapofika 25 july itakuwa imetimiza mwezi tangu Audio kutoka lakini pia tar 25 july Baghdad & Jo Gift watakuwa wakitimiza mwaka mmoja tangu wahalalishe mahusiano yao yaani wakiwa katika ndoa. Baghdad amesema ya kuwa siku ya tar 25 yeye na mke wake wataachia wimbo kama zawadi kwa familia ndugu jamaa na marafiki ambao wengine wamekuwa nao bega kwa bega katika kushiriki ndoa yao kuwa imara siku hadi siku.

Baghdad “ndoa ni maamuzi na sio fashion sisi tunatimiza mwaka kwenye ndoa lakini kwenye mahusiano unaenda mwaka wa 4 changamoto zipo lakini kikubwa kilichoweza kunisaidia tangu awali nilichukua mapungufu ya mke wangu na kuangalia jinsi ya kumrekebisha nae vivyo hivyo mpaka leo nashukuru mungu naweza sema ni saiz yangu kwa maaana kumpata mtu ambae atakuwa vile unataka haiwezekani bali ukiamua kumtengeneza ni kazi rahisi na ki ukweli ninamshukuru saana mungu kwa zawadi ya mtoto aliyonipa KYLE Tunampenda saaana na kila nikisikia minong’ono ya kuwa wanatuhesabia siku huwa nazidisha kusugua goti kwa Mungu kuzidi kuomba ulinzi juu yetu na rehema zake maana tulikuwa tukiesabiwa wiki ikaja miezi ikaja mwaka sasa hivi wanabaki kusema ndoa ndoano watayakanyaga tu bt I don’t care b coz najua vile tunamshirikisha Mungu katika maisha yetu

Aidha Baghdad amesema ya kuwa tar 31 july atazindua video yake maeneo ya CHIMBO INC iliyopo karibu na hospitali ya KAIRUKI mkabala na CHAIDERS REC mikocheni kwa namna tofauti.

Uzinduzi huu sijalenga kupata hela no lengo ni kukutana na watu wanaopenda mziki wangu wanaosaport kwenye mitandao ya kijami na sehemu nyingine kukaa kuiona video kwa mara ya kwanza kabla ya tar 1 august kuingia mtaaani na kwenye vyombo vya habari. Mlangoni mtu atakapoingia atapewa DVD yenye CD 2 moja ikiwa na Video na Nyingine Ikiwa ni KANDA MSETO yenye nyimbo 10 nilioipa jina ya VYA ZAMANI NI DHAHABU ambayo nimerudia nyimbo za wakongwe. Ukiingia ndani utapata nafasi ya kusosomola kuku nyama ya ng’ombe ya kuchoma ndizi na kuku vyote hivyo kwa gharama ya shilingi elf 10 tu.

Uzinduzi utaanz saa 12:30 jion na kuisha saa 6 kamili usiku jinsi ya kupata ticket ni kwa njia ya simu utatuma pesa yako yenye thamani ya elfu kumi kwenye number 0652 89 48 71 kisha utapewa ID number ambayo ndio itakuwa ticket yako siku ya tukio. kutakuwa na watu wengi mashuhuri wengi sana waliojitolea kuja kumsport Baghdad pamoja na vyombo mbalimbali vya habari.

Kwa maelezo zaidi waweza kuwasiliana na mratibu wa shughuli nziima kwa number 0652 89 48 71 au kwa kumfollow instagram @bagh_dad ama e mail bdady2009@gmail.com.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez