‘Subira yavuta kheri’ Mkubwa Fella

‘Subira yavuta kheri’ Mkubwa Fella

Said Fella maarufu kama Mkubwa Fella ambaye ni moja kati ya wadau wanaomiliki wasanii wengi katika ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Mapema leo hakusita kuonyesha nyumba ambazo amewakabidhi vijana wake wa Yamoto Band, Ambapo nyumba hizo zinafanana kwa kila kitu.

Mkubwa Fella amesema “Nimeamua kuwaonyesha waandishi wa habari nyumba hizi ili kutoa maneno maneno. Maana wapo ambao husema hawana kitu, ila wakumbuke Yamoto Band wana miaka mitatu tangu waanze. Na leo hii nawakabidhi nyumba zao zenye gharama, hizi sio vibanda ni nyumba. Hivyo watu wajue subira yavuta kheri, subira waliyovuta vijana wangu ndio hii sasa.

Pia mkubwa Fella hakusita kueleza vijana ambao anao sasa katika kituo cha Mkubwa na Wanawe ambapo amesema “Mpaka sasa nina vijana 110 na wote nina wahudumia kwa usawa.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez