STEVE NYERERE,DUDE NA WILLIAM MTITU NITAKUFA KWA MAPENZI YA MUNGU.

stive nyerere
Muigizaji Steve Nyerere ambaye alipata umaarufu zaidi kwa kuwa na uwezo wa kuigiza sauti ya baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere,Amabye kwasasa anafanya vizuri katika tasnia ya filamu hapa inchini Tanzania.
Katika hali isiyo ya kawaida Stephen Mangere maarufu kama Steve Nyerere ameandika maneno makali katika ukurasa wake wa instagram,ambapo alisema”Naomba kumshukuru kwa kila jambo yehova wewe ndio kimbilio langu.Pili kwa masikitiko makubwa nasema watashindana ila hawata shinda niongee kidogo kwa ufupi mara kwa mara nimekuwa nadhalilishwana najiuliza tatizo nini nagundua nyota.Maishani kila binadamu mungu kampa fursa yake so ukubali ukatae ndio hivyo.Nilipigiwa simu na Mrs Adam Kuambiana yani mke wa marehemu kama rafiki ndugu na msaniimwenzake kuwa anajenga kaburi la marehemu Kuambiana,nikajiuliza kwanini ajenge na sisi tupo wapi?tuliokuwa tunakunywa nae tunacheka nae ,nikamuomba mke wa marehemu Adam tuchangie kama wasanii wenzie akakubali.Baada ya hapo nilibeba jukumu hilo,nikampigia Jb akasema anachangia laki tatu,nikampigia MH Makonda akachangia laki saba jumla tukapata milioni moja na kumkabidhi mke wa marehemu.So mpaka siku ya misa mke wa marehemu Adamu alinishukuru kwa msaada huo tatizo langu liko wapi?Akatoka Dude akatokea na kusambaza Dude na wenzako mnajijua naomba kukwambia na kuwaambia tz wenzangu kuna kundi la watu watano 5 tena wasanii wanatamani Steve Mengere afe leo wanahangaika huku na kule Dude nitakufa kwa mapenzi ya mungu Mtitu nitakufa kwa mapenzi ya mungu.Mnatoa hela kwa waandishi wanichafuekwenye mitandao hahaha.Kauli yangu wabaya watu wazuri watu samba hawezi toka Serengeti akaja mjini kukualibia.Mti wenye matunda ndio hupigwa mawe wasanii hamuwezi kuwa wamoja hata siku moja kwa roho mbaya mlio nayo bra kumfadhili mbwa msanii wa movie hana shukurani hata kidogo.Ipo siku umuhimu wangu mtaujua mungu ni mwema kwa kila jambo.
Hata hivyo William Mtitu nae aliamua kumjibu kupitia ukurasa wake wa isntagram nay eye alisema”Da!Naomba ndugu zangu mnisamehe kwa kuandika hili humu instagram .Maana lilitakiwa liongelewe nje ya haopa kiukweli Steve nimestuka sana baada ya kuona post yako tena umenihuzunisha sana kunitaja kwa jina katika ugomvi wako na Dude nimejaribu kukupigia simu hupokei simu zangu na umsema kuwa natamni ufe.Hivi tujiulize ndugu yangu?so ukifa mimi Napata faida gani?kwani mimi nina ugomvi gani na wewe?kwanza tunafanya vitu tofauti mimi ni producerna msambazaji wewe ni mchekeshaji kwanini nigombane na wewe?kwanini Steve hutaki kujifunza mdgogo wangu maneno haya haya yamesababisha Kanumba amekufa huku haongei na Ray wakati walikuwa marafiki kwa zaidi ya miaka kumi na Kanumba amekufa huku akiwa na bifu kubwa sana na wewe ahdi anakufa hamkuwa mnaongea kwasababu ya haya hya maneno yako.Kuwa na amani Steve wewe ni mhehe kama mimi kwetu ni kumoja miongoni mwa watu ambao sitawasahaukatika maisha yangu wewe ni mmoja wao,umenisaidia vitu vingi sana nakuhukuru Mangere.Pamoja ulapa ukiwa na matatizo nisije mimi nitakuja tu labda wewe kama unahisi mimi mbaya wako umekosea mimi sina ubaya na wewe kabisa na sioni sehemu pakutugombanisha maana hatuna tunapokutana gud day bandugu”.Aliandika.