Stereo Atoa ushauri kwa wasanii

IMG_3286

Stereo Atoa ushauri kwa wasanii

“Sana” ni wimbo wake unaofanya vyema katika vituo vya radio mbalimbali hapa nchini. Stereo aliwahi kufanya vyema zaidi na nyimbo kama, Mawaidha,Rafiki,Chundabadi, Confidance pamoja na nyingine nyingi.

Mapema leo hakusita kuiambia tizneez.com juu ya kile kinachoendelea kwa wasanii wa hiphop ambao ni chipukizi kuonekana kukosoa mara nyingi hasa katika hoja zisizo na mashiko. Stereo amesema “Naona awatu mnagawanywa na muziki,niliongea hili siku za nyuma wivu,majungu, fitna, chuki, havitatufikisha popote. Aliye juu atabaki kuwa juu na aliye chini anaweza pia asifike juu pia.

Ni vyema kuzingatia busara na kupenda kujifunza bila kusahau kuheshimu watu waliokuinspire uchane, focus fanya ngoma kali ili usikike na watanzania na kuinspire wadogo zetu wengine. Huu ni sawa na mchezo wa vijiti, leo huyu kesho yule. Usela mavi hauna dili tufanyekazi kwa bidii,tusome kwa bidii,tusali kwa bidii,na tusaidie wasiojiweza.Tujijengee mazoea ya kupata umaarufu kwa kazi nzuri tunazofanya na si kwa kuzungumzia wengine vibaya ilimradi tu baadhi ya watu wajue kwamba na sisi tumo. Tukizingatia haya tufakika mbali muwe na siku njema.”

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez