STAMINA LIKE FATHER LIKE SON NI MIPANGO ENDELEVU

0
Rapper kutoka Moro town Stamina ambaye ni kinara wa mashairi katika muziki wa hip hop hapa inchini Tanzania. Stamina ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa like father like son remix aliyowashirikisha wakali kama,Chid Benz,Fid Q,Nikki Mbishi,Songa na Noorah. Stamina aliambia team tizneez”Mwanzoni nikiwa natoa ngoma yangu ya Like father like son niliyofanya na Fid Q tayari nilikuwa na maamuzi mengine kichwani,hii remix sio imekuja ghafla hapana ni kitu ambacho kilikuwepo tangu nafanya version ya kwanza. Na hii ndio sababu ya kutokufanya video ya version ya kwanza,hivyo ijumaa ya tarehe 21/8/2015 tunaanza kushoot hii remix.Na kwa faida ya wasiojua hii itakuwa ni video ya kwanza ya wimbo wa remix kwa hapa Tanzania.Zimewahi kutoka remix nyingi ila hazijawahi kutoka video yake kwaiyo ni mipango endelevu tangu nafanya wimbo huu nilitaka iwe hivi. Hata hivyo stamina hakutaka kuweka wazi kwamba video hiyo inafanywa na director nani.Ila Alisema”Mashabiki wangu wakae mkao wa kutazama video nzuri yenye script kali na ya kijanja. Unaweza kuwa rafiki yetu faceboo.com/tizniz instagram.com/tizneez twitter.com/tizneez