Stamina Apiga hatua nyingine katika uelekeo wa maisha ya ndoa

Stamina Apiga hatua nyingine katika uelekeo wa maisha ya ndoa.

Msanii wa muziki wa hiphop Stamina siku ya jana alipiga hatua nyingine katika uelekeo wa maisha ya ndoa.

Ambapo 27.4.2018 Jijini Dar es salaam kumefanyika sherehe ya uago katika upande wa mwadadada ambaye ni mchumba wake na Stamina.

Sherehe ya uago ni katika tamaduni ambazo hufanywa kwa upande wa mwanamke ili kuonyesha heshima ya kuagwa katika kwenda kuanza maisha mapya ya kaya yake.

Na katika sherehe hiyo Roma na Mkewe ni miongoni mwa wengi walioudhulia, ambapo Stamina amethibitisha ndiyo watakuwa wasimamizi katika siku ya kufunga ndoa yake mnamo 5.5.2018

Team Tizneez twakutakia yote yenye kheri katika maisha mapya yenye upya wa uhalisi wa kila mwanadamu mwenye kujua thamani ya ndoa.

Pongezi ziwe na wewe Stamina katika hatua hii. Na hakika “Aonjae asali, huchonga buyu la asali”

 

Baadhi ya picha katika sherehe hiyo ya Uago wa mchumba wake na Stamina

 

 

 

#TuzungumzeMuziki