SOGGY DOGGY SITAFICHA HISIA ZANGU KISA NIFURAHISHE MIUNGU WATU

index
Soggy Doggy Hunter ni moja kati ya wakongwe wa music wa bongo fleva, ambaye amewahi kufaya vizuri na ngoma zake kama kibanda cha simu,story,kulwa na doto,nilikaona mwaka jana pamoja na nyingine nyingi.
Soggy licha ya kuwa rapperlakini pia ni mtangazaji wa kituo kimoja cha radio hapa Jijini Dar es salaam.Soggy hakuficha hisia zake kwa mashabiki baada ya kuamua kusema”Tambueni hili hisia zangu kwenye siasa sitaziacha kisa nifurahishe miungu watu,mnaotaka wote tuwe CCM jiulizeni wenyewe kwanini ulianzishwa mfumo wa vyama vingi?mimi ni Chadema tena mwanachama sio shabiki.Kama wewe ni ccm na hupendi ninachopost na ukatumia mwamvuli w kuwa mimi ni mwanamuziki basi ujue nitakupa jibu usilolipenda,hata kahaba anaongelea siasa sembuse mwanamuziki?wengine utawasikia et ooh umefulia hawa huwa wanifanya nicheke maana wakati naanza muziki nilikuwa na plan A,B=na C za maisha yangu.Bila muziki naishi na kusomesha wanangu,nashangaa kama utakuwa bize ku-dis wakati hunilipii hata bundle na wala sikuombi unifollow.Niacheni na maisha ninayoishi ukitaka tuelewane leta deals tupige pesa sio blahblah zisio na kichwa wala miguu kwenye post zangu au ndo hapa kazi mnayosema yamenifika koromeoni.”
facebook.com/tizniz
intagram @tizneez
twitter @tizneez