Soggy Doggy Asema Watu kama Jebby ni wachache mno.

Soggy Doggy Asema Watu kama Jebby ni wachache mno.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Jebby kabla ya kupatwa na mauti ameugua takribani wiki mbili.

Ambapo alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu, lakini uvimbe kwenye bandama.

Na Jebby amefariki leo 22.4.2018 Mkoani Dodoma. Na shughuli za mazishi ziko nyumbani kwako Area C Mkoani Dodoma.

Na kwa mujibu wa msanii mkongwe Soggy Doggy anasema “Jebby anaweza akazikwa kesho, niwaombe watu wa Dodoma wajitokeze kwa wingi kwenye msiba wake.

Watu kama Jebby ni wachache mno, hivyo watu wawape nguvu wazazi wake na ndugu zake”.

Pumzika kwa Amani Jebby.

#TuzungumzeMuziki