“Siwezi kukubali kutukaniwa mama yangu na wajinga wajinga” Sugu

IMG_2828

“Siwezi kukubali kutukaniwa mama yangu na wajinga wajinga” Sugu

Freedom ni wimbo wake unaofanya vyema katika vyombo vya habari kadhaa hapa nchini. Joseph Mbilinyi aka Sugu ni mbunge wa kwanza kutoka kwenye muziki wa hiphop kuweza kuchaguliwa na wananchi kuwa mbunge katika Jimbo la Mbeya Mjini.

Mapema leo kumekuwa na taarifa zinazosema”Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson ameitaka Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuchunguza tuhuma dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi anayedaiwa kuwaonyeshea kidole cha kati wabunge wa CCM.
Sugu anadaiwa kufanya kitendo hicho June 6, mwaka huu alipokuwa akitoka katika ukumbi wa Bunge”

Kupitia mtandao wa picha MH Joseph Mbilinyi ameposti maneno yanayonekana kama picha ambayo yanasomekana “My take, wanazungumzia sugu kuonyesha wanachoita dole la kati. Lakini hakuna anayezungumzia zomea zomea na matusi ya nguoni dhidi yangu, siwezi kukubali kutukaniwa mama yangu na wajinga wajinga tu waliovaa joho la uheshimiwa mle bungeni. Mbunge wa ccm hawezi kuniambia toka nje k@m@k***harafu mimi nitoke bila reaction yoyote ile!!Not Me!”

ambapo pia alimalizia kwa kuandika maneno katika picha hiyo  yakisema “The Most Voted MP # FREEDOM to express myself…

HIVI NDIVYO JINSI TEKNOLOJIA INAVYOPIGA TAFU MZIKI WETU

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez