SISTER P,AELEZA SABABU ZA P FUNK KUMKUBALI

hqdefault

Sister P ni moja kati ya waasisi wa muziki wa hip hop kwa upande wa kike.Licha ya kuwa muasisi wa muziki wa hip hop lakini kwasasa amebidilika na kuimba aina nyingine ya muziki ambao ni mchiriku huku akiwa ameshirikisha mkali Msaga Sumu.

Akiongea kwenye kipindi cha The Jump Off cha Times fm kinachoongozwa na Jabir Saleh,Sister P alisema”haikuwa rahisi kufanya kazi kwa P funk kwa miaka ile ya 2002,lakini kilichofanya P Funk anikubali zaidi ni kukosekana kwa rapper mzuri wa kike kwa kipindi kile,  Ambapo kwa wakati ule alikuwepo Zay B.

Anakuja,mr dj,wanachonga juu yangu,ni baadhi ya nyimbo zilizompatia umaarufu mkubwa Sister P miaka ya nyuma.

Unaweza kuwa rafiki yetu facebook.com/tizniz

instagram.com/tizneez

twitter.com/tizneez