Siku ya wanawake Dunia ilihali yapasa wimbo wa Ay ukae vichwani mwenu.

Siku ya wanawake Dunia ilihali yapasa wimbo wa Ay ukae vichwani mwenu.

#MwanamkeNiSikuZote

Hakika mwanamke ni siku zote maana katika uhalisia Dunia ingekuwa mbaya kama tungekosa uwepo wa wanawake. Maana katika kweli umuhimu wao ni kila wakati katika sehemu zote.

Hivyo kwa kufikiri nguvu yao, umuhimu wao wa kila wakati ndiyo uhalisia wa kuanzia neno la #MwanamkeNiSikuZote

Na katika histori siku ya mwanamke ilianza kwa kuitwa siku ya wafanyakazi wanawake, na nyakati zote hukumbukwa kila mwezi wa 3 tarehe 8.

Na dhumuni kuu la siku hii ni kuonyesha upendo na heshima katika kile pande ya mafanikio yake kupitia kazi mbalimbali kama muziki, siasa, utangazaji, ujasiriamali na kazi nyingine Nyingi.

Na rasmi siku hii ilianza rasmi 8/3/1857 na leo tena 8/3/2018 tunaikumbuka siku hii.

Na kwakuwa Tizneez ni uwanja wa muziki hatuachi kusema yakuwa #MwanamkeNiSikuZote. Lakini hatuachi #TuzungumzeMuziki.

Wimbo wanawake watafutaji wa Ay akiwa na Stan Boy ukakae vichwani wanawake wote. Maana wimbo huu una kweli yenye kupaswa kusikilizwa na wanawake wengi Zaidi.

Katika wimbo huo Ay ameongea mengi ya kumjenga mwanamke ambapo kuna mahala anasema “Unaehangaikia maisha yako, nakukubali kinoma”

Ay anaongeza tena kwa kusema “Wengine wanachapa buku na kazi pamoja, wengine wapo mtaani wanagombania kutoka” hakika ni mwanamke mtafutaji.

Wimbo huu unabaki kuwa funguo kwa wanawake wote. Na sisi twasema #MwanamkeNiSikuZote

Utazame hapa wimbo huu

 

 

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa