Siasa si maisha? Kwanini wasanii wasiimbe maisha?

Siasa si maisha? Kwanini wasanii wasiimbe maisha?

Kumpangia msanii cha kuimba ni kuweka mipaka kwenye kipaji chake. Lakini ni wazi katika uhalisia hakuna jambo baya kama kupangia mtu kitu cha kufanya, hasa msanii kwenye kazi yake ya Sanaa. Kauli ya waziri inaleta mashaka mno kwa watu wenye mitazamo ya kuona mbali.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Harrison Mwakyembe Amesema “Ni marufuku kuimba nyimbo za siasa” Mh ametoa kauli hiyo leo Bungeni Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mh Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya.

“Tuzungumze muziki wetu”

Muziki ni sehemu ya burudani lakini pia muziki ni sehemu kubwa ya kufungua watu na kuwatoa katika utumwa  Fulani au kuwaokoa katika jambo Fulani. Miaka ya nyuma wakati wa kudai haki (Uhuru) nchi nyingi zilitumia Zaidi wasanii kutunga nyimbo za kuhamisha.

Leo wanapigwa marufuku katika tungo hizo kwanini? kipi ambacho kinafichwa? Lakini wasanii hawa ndio hutumika kuimba nyimbo za miaka ya 50 ya uhuru au hata kuimba nyimbo za kampeni wakati wa uchaguzi. Je!ile sio siasa? Kwa umuhimu wao ndiyo maana wanatumika kipindi cha kampeni, hivyo basi tuone umuhimu wao na umuhimu wa tungo zao za siasa hata baada ya kampeni. Naamini tungo zao zipo kwaajili ya kukumbusha mema yanayopaswa kufanywa katika kuokoa Sanaa yao na hata maisha mengine ya wanajamii.

Leo hii Mh Waziri kupiga marufuku tungo za kuimba siasa ni wazi amekuwa anawapangia wasanii aina ya muziki wa kufanya. Je wasanii wote waimbe nyimbo za mapenzi pekee?. Je tutakuwa tunajenga Taifa la namna gani?

Lakini si kuna uhuru wa kuongea? Ila jambo baya ni kuongea na kuvunja sheria. Kuna mengi ya kufanya katika muziki huu wa kizazi kipya ili vijana waendelee kujikomboa kimaisha kupitia vipaji vyao. Kuwakewa mipaka sio jambo lilolojema, ila jambo jema ni kuwakumbusha kuwa wawe na tungo zenye ukweli.

Kama tunataka kukuza Sanaa yetu basi tusiwapangie wasanii wetu cha kuimba katika kazi yao ya Sanaa.

Bali tuwakumbushe kuhusu sheria na taratibu za kuzingatia katika kazi yao ya Sanaa.

Mungu ibariki Sanaa ya muziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa