SHILOLE TUJIFUNZE KUWA NA SHUKRANI

Shilole

SHILOLE TUJIFUNZE KUWA NA SHUKRANI

Shilole ni moja kati ya wasanii walio kuwa katika tasnia ya Bongo Muvi na kuhamia katika muziki na kupata mafanikio makubwa.

Nakomaa na jiji, chuna buzi hizi ni baadhi ya nyimbo zake zilizofanya vyema katika media mbalimbali, ambazo ni wazi zimempatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Shilole ameweka wazi mtazamo wake juu ya watu waliowengi, ambao katika maisha wamekuwa wakizungumza mabaya zaidi kuliko mazuri ya mtu. Shilole alisema “ni vyema kujifunza kuwa na shukrani kuliko muda mwingi kutumia kumsema mtu vibaya tena baada ya kuvunja mahusiano ya kimapenzi. Hivi fikiria uko na mtu ambaye kila siku anafua nguo zako au kila asubuhi anakuandalia chai pamoja na mengineyo lakini mkiachana unasema hakuwa mtu mzuri kwako, hapana jifunzeni kuwa na shukrani maana hata Linah aliwahi kuimba wimbo unaozungumzia shukrani.”

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez

 

 

 

 

 

 

Source Twenzetu Times Fm