Shilole Nawaza mbali sioni faida ya kiki za mitandaoni

shil

Shilole Nawaza mbali sioni faida ya kiki za mitandaoni

Ni moja kati ya wanamuziki machachari ambaye penzi lake na kijana mdogo Nuh Mziwanda lilifanya wakazidi kupata umaarufu kupitia mitandao ya kijamii, hasa katika kile walichokuwa wanakionyesha katika kurasa zao hasa mtandao wa picha “Instagram”

Shilole akiongea na Team tizneez kwa njia ya simu amesema “Nimekuwa na najitambua hivyo sasa sihitaji kiki za mitandao bali nawaza mbali zaidi ya hapa. Hivyo sio rahisi mimi kumjibu chochote yule anaekuwa ananizungumzia katika mitandao ya kijamii, maana niliwahi kufanya hivyo na sijaona faida yake.

Lakini pia sasa nipo na msanii wangu Gaucho na nimeamua kumsaidia katika mlengo wa kufanya biashara. Na pia naomba support yenu kwa Gaucho.”

Team tizneez haikusita kumuuliza Shilole juu ya album ambapo alisema “Sina mpango maana hakuna faida yoyote lakini kama ikitokea kuna faida inapatikana basi nitafanya maana tayari nina nyimbo nyingi”.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez