“Shilole kupigia simu wasanii analia huo ni uchawi” Nuh Mziwanda

IMG_20150719_083323

“Shilole kupigia simu wasanii wenzangu huku analia huo ni uchawi” Nuh Mziwanda

Jike shupa ni wimbo wake Nuh Mziwanda ambao sasa unafanya vyema katika vituo mbalimbali vya radio na runinga hapa nchini

Akiongea na team Tizneez Nuh hakusita kuweka wazi hisia zake ambapo alisema “Kwanza nifanye kiki ili iweje?sifanyi kiki nafanya muziki mimi nauza nategemea kazi yangu ndio iuze, lakini nahisi nipokuwa nafanya mahojiano na kuzungumza vyema labda anaiona mimi mjinga.

Lakini mimi sijafundishwa kugombana na mtu wala kurumbana, hasa kwa mtu kama yeye ambaye ni msichana wangu wa zamani. Yeye hakuwa na sababu ya kumpigia simu dj wa Iringa eti asipige wimbo wangu. Pia hakuwa na sababu ya kumpigia simu kuwataka wasanii wafute post ya video yangu maana ninamdhalilisha kwenye ile video huku analia huo ni uchawi na hiyo ni roho mbaya.

Nahisi hakutegemea kama nikitoka kwake alijua sitaweza kuendelea kwenye muziki wangu na kufika sehemu ninayotaka ila ajue kama kuna mungu. Na nahisi kutokuwa na kinyongo nae ndio maana mambo yangu yanafunguka.

Kiukweli nimesikitishwa na hili jambo na ni jambo baya .Ila me nataka aendelee vyema katika kazi zake maana ni wazi anafamilia na anategemea ila nashangaa yeye hana huruma na mimi.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez