SHAIRI MAALUM KWA JOHN WALKER By Wagosi wa kaya

IMG_2035

Siku moja baada ya kifo cha msanii John Walker ambaye pia alikuwa mtu wa karibu na kundi la wagosi wa kaya tokea mkoani Tanga, Mapema leo Msanii Mgosi Mkoloni moja kati ya muanzilishi wa Wagosi wa kaya amemuandikia shairi maalum rafiki yake na ndugu yake John walker

Ilikuwa jumapili/jioni saa kumi na mbili
Uchovu wa mwili/nasafiri kikafiri
Kumbe zilikuwa dalili/ubovu umeshamiri
Zaidi ya mara mbili/gari ugonjwa linabadili

Kukatika kwa mikanda/injini ikasimama
Hofu ikaanza kutanda/porini nilikwama
Nikatoka kikamanda/hapo jua linazama
Vipimo vikapanda/gari inachemsha kiama
Giza nalo likatanda/nawasha simu nipate mwanga kutazama
Ujumbe mzito ukapanda/Jcb ananiuliza hii habari umeitazama?
Nilihisi moyo utaganda/ukimya ukatanda

Msata mpaka Dar/masaa 6 utashangaa
Sikula sikuhisi njaa/marafiki walinishangaa
Nilipiga simu kadhaa/sikulala sikukaa/niko wima kama kichaa/jumatatu asubuhi kukakucha

Mbio muhimbili/nikawaona wazazi pole wakazipokea
Wala haikuwa siri/kitandani nikamsogelea
John Woka umelala/najua punde utaamka
Tupige story za Mtwara/kwa pamoja tukicheka
Niliongoza sala wakati umelala/kupumua kwako ilikuwa ni ishara
Bado tupo pamoja/mimi na Papaya tupo kwa nje tunakungoja
Ras Lion toka safari/akaingia kukuona
Alipotoka nje ukaondoka bila neno kusema

Mama akiniona/anahisi na wewe utatokea
Baba nikimuona/kuna jambo ataongea
Nakosa nguvu napomuona mkeo/John Woka umeniliza juzi jana na leo
Umetuacha na wanao/mashabiki na ndugu
Majonzi kila uchwao/Mtaani vilio na uchungu

Umekwenda kweli/wagosi hatuamini
Hivi hii ni kweli/leo hauko na mimi?
Bwana amekuchagua/ajali ni kama njia
Hakuna anayejua/nini kipo kwenye njia
Daima utakumbukwa/uwezo na kazi zako ni kitu kikubwa
Unarudi kupumzika kwa baba aliyetuumba.
Asante John Woka……..umekwenda
Michael Denis Mhina………..umekwenda rafiki…..

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez