Shabiki wa Albert Mangweair awandikia ujumbe Clouds Media Group.

Shabiki wa Albert Mangweair awandikia ujumbe Clouds Media Group.

Habari Team Tizneez najua ukubwa wenu sasa katika upande wa blog ambazo zinaandika kuhusu Bongo Fleva/Hiphop, kiukweli mnafanya vizuri katika chambuzi zenu ila nashangaa kuona mpo kimya katika chambuzi ya Clouds kumpandisha Mama Mangweir jukwaani.

Kiukweli nilitegemea kuona mkisema kitu, ila ukimya wenu umefanya nihoji juu yenu je na nyie mshanunulia kama wenzenu wengine Bongo 5. Nawapenda kwa kuwa mko tofauti na wengine mmesimama katika ukweli zaidi bila kujali nani ni nani kwenye muziki wa kizazi kipya.

Wacha nirudi katika lengo langu juu ya kuandika ujumbe wangu kwenu nyinyi na kuamua kuwatumia na sio kuandika katika mitandao ya kijamii. Najua hapa wengi watasoma sio katika page za mitandao ya kijamii. Katika mitandao ya kijamii wengi hudharau maoni yetu sisi mashabiki na wengi hudhani wewe ni mpuuzi ambaye umeandika maoni.

Kukweli mimi ni shabiki wa Ngweair tangu kutoka kwa wimbo wake wa Ghetto langu, mpaka wimbo wake wa mwisho wa No Beef.

Kifo chake ni moja kati ya vifo vichache vilivyonigusa katika wasanii tangu kuanza kuwa shabiki wa muziki . Nimeona Fiesta ya juzi pale katika Mji wa Morogoro team nzima ya Clouds Media pamoja na wasanii husika walipotembela nyumba ya milele ya Ngwea, kimsingi si jambo baya ni jambo jema ingawa naona wanajali thamani yake baada ya kufa na sio alivyokuwa hai.

Ila katika mambo ambayo yamenisikitisha ni jambo la kumpandisha mama jukwaani, kwangu ni jambo baya zaidi. Huenda kwa hekima za mama ameshindwa kukataa ila katika uwazi tazama umri wa mama je ni kweli kulikuwa na haja ya kumpandisha jukwaani?

Jambo hili hata jamaa angekuwepo ni wazi asingefurahishwa nalo, maana tangu nianze kuwa shabiki wake sijawahi kuona akimuonyesha mama ake kwenye media wala kutaka mama ake azungumze juu ya muziki wake.

Yaweze kuwa sasa mnampa msaada mama ngwea ila sioni haja ya kummulika zaidi na makamera yenu pamoja na picha lukuki katika mitandao ya kijamii. Naona mnamchoresha Bi mkubwa mkizingatia hata Majani alisema nyinyi ni chanzo cha mawazo juu Ngwea mpaka kupelekea kifo chake.

Thamani ambayo mnamuonesha Ngwea onyeshi basi kwa wengine ambao wako hai, mfano mlivyokuwa moro sikusikia habari yoyote kuhusu Afande Sele ingawa najua yupo, ila najua ikitokea hayupo mtaanza kusema ooh mfalme wa Rymes pekee. Mambo haya mimi kama shabiki sipendezwi nayo, unafiki umekuwa mkubwa kuliko uhalisia wa jinsi ambavyo mnaishi.

Napenda kuwashauri ingawa najua ni wajuaji kuliko wengine na huwa hampendi kuambiwa ukweli ila ni vyema mkamuacha mama wa watu ajipumzikie na sio kumpandisha katika majukwaa yenu,  najua faida ya kumpanisha jukwaani kwa upande wenu ni kubwa maana ni watu wa kutaka kuonekana mmefanya kitu juu ya jambo Fulani au mtu fulani

Ila tazame tena umri wa mama na kitendo cha kumpanisha jukwaa na mnajua shoo zenu jinsi zilivyo matusi na makundi ya wahuni kutawala, kwangu naona mmekosea mama wa watu ni vile anashindwa kuweka wazi. Ila jitazameni tena na tena mimi kama shabiki wa ngwea sijapenda na naomba msifanye kitendo kile.

Fikirini kabla ya kutenda tafadhari jamani naona mnachoresha bi mkubwa tu.

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez