SAM WA UKWELI “MKATABA ULINIINGIZA KWENYE MATATIZO”

index
Sam wa ukwel ni miongoni mwa wasanii waliotokea miaka ya 2010 na kufanya vizuri na wimbo wake wa sina raha,licha ya kuwa na nyimbo kama.samaki,hata kwetu wapo,usiniache mchumba na nyingine nyingi.
Takribani miaka 4 Sam amekuwa kimya katika kazi zake za music,Mapema leo akiongea kwa njia ya simu na team tizneez Sam wa ukweli alisema”Nipo kimya nalitambua hilo,lakini kitu kimoja wapo kilichofanya niwe kimya ni mkataba,niliingia mkataba na aljazira ambao ndo walikuwa wanasimamia kazi zangu.Lakini sikuwa kisheria kwa upande wangu,kwahiyo baada ya muda nikawa nabanwa zaidi na baada tukawa hatuna maelewano baina yangu na yao.Na kwakuwa sikuingia kisheria sikuwa na chochote cha kufanya,ila sasa mkataba umeisha kama mwezi mmoja hivi na tayari nimeshafanya ngoma kadhaa na nimeenda mpaka nairobi kutafuta director wa video.Hivyo ninarudi rasmi kwenye game.Ila mkataba wangu uliniingiza matatizo tu.”Alisema
Mwisho.
twitter@tizneez
instagram@tizneez