Sallam Sk ‘’Ommy Dimpoz anamjua Zaidi Diamond kuliko ninavyomjua mimi’’

Sallam Sk ‘’Ommy Dimpoz anamjua Zaidi Diamond kuliko ninavyomjua mimi’’

Meneja wa Kimataifa wa Mwanamuziki Diamond Platnumz, Sallam Sk amefunguka kwa kusema kuwa Muimbaji Ommy Dimpoz anamjua zaidi Diamond Platnumz kuliko yeye.

Akiongea kupitia kipindi cha Campus Vibes cha Times Fm jana usiku, Meneja huyo amedai kuwa hawawezi kuingilia tofauti walionayo Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz kwa kuwa Wanajuana kitambo kabla yake.

“Mimi huwa naweka sana utani mitandaoni, Ommy Dimpoz anamjua Diamond zaidi kuliko mimi, sio kumbembeleza eti Ommy amuombe msamaha Diamond kwa faida gani hasa ninayoipata au nitakayopata kutoka kwake? aende mwenyewe akaombe Msamaha” alisema Sallam.

Katika hatua nyingine Meneja huyo ambaye kwa sasa amejipa jina la Rais wa Zimbabwe Mugabe, amewataka wasanii kwenda kwake kama wanataka washirikiane kibiashara na si kuomba msaada.

Source Times Fm

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa