Sababu ya wasanii kukosa mapokezi ya “BASATA” wanaposhinda tuzo za kimataifa

Image00012-1

Sababu za wasanii kukosa mapokezi wanaposhinda tuzo za kimataifa

Kumekuwa na malalamiko mengi ya juu ya mashabiki ambapo hutoa shutuma kwa Basata juu ya kutokuonekana katika mapokezi ya wasanii mara wanapokuwa wameshinda tuzo za kimataifa.

Msemaji wa Basata Ndugu Arestide Basedya hakusita kuweka wazi ambapo alisema “ Kuna mengi yanasababisha Basata na vyombo vingine vya Serikali kuto kutokea katika hayo mapokezi. Ila kikubwa huwa wasanii wanaondoka bila kufuata taratibu, nadhani kuna haja ya menejimenti zao kuelimishwa juu ya hilo. Hili si la wasanii pekee ila hata wana michezo.

Unapokuwa unaondoka kwa utaratibu lazima Serikali kupitia kwenye chombo husika lazima ikupe bendera ikimaanisha unakwenda kuwakilisha taifa”

Ni vyema sasa wasanii wetu na wana michezo wote kufuata taratibu ili muweze kupata mapokezi mazuri kutoka kwa Serikali yetu yenye kujali nafasi ya sanaa kwa ujumla.

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez