Romy Jones na Baraka Da Prince wote ni vipofu hakuna wa kumuongoza mwenzake.

Romy Jones na Baraka Da Prince wote ni vipofu hakuna wa kumuongoza mwenzake.

Hakika “Wapumbavu huchukia maarifa” bali wenye utashi hupenda.

Utambuzi wa maarifa hufanya mtu kufikiri, bali asiye na maarifa huendeshwa na upumbavu ilihali hukumbana na fedheha ya wajuzi.

Hakika mswahili hakukosea yakuwa “Kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake, hakika wote watadondeka shimoni”.

Na huu ndiyo uhalisi wa hawa ndugu zetu ambao wapo kwenye sanaa ya muziki wa kizazi kipya yani Baraka Da Prince na Romy Jones.

Wiki kadhaa nyuma walianzisha zogo katika mitandao ya kijamii, hasa katika hali ya kuleteana kashfa na mengi yasiyo na maana bali hovyo.

Na yupo mmoja wa mashabiki ambaye hatuna hakika na utashi wake ambapo alituuliza kwa lugha kali “kwanini tuko kimya katika kuweka swala hilo la hovyo?

Hakika hatukuwa na jibu juu yake, bali kutafakari yakuwa hajui kwenye muziki kuna mengi ya kuzungumza kuliko zogo la hovyo ambalo kwa maono ni kiki ya wimbo. (Uhalisi)

Katika uhalisia Romy na Baraka hawa ni watu wa wasanaa ambao mioyo yao imepondeka kwa kuamini yakuwa huwezi kutoa wimbo mpaka ufanye tukio la hovyo. (Kiki)

Lakini hili linatokana na kifungo cha ufahamu juu yao. Hakika “Hakuna kifungo kibaya kama cha ufahamu”

Na kifungo cha ufahamu kimezaa zao la kiki ya kutupiana zogo la hovyo kwenye mitandao, na nyakati hizi wanasema yakuwa wanatoa wimbo wa pamoja na ni katika hali ya kumaliza tofauti zao.

Hakika “Ni kheri mrama kuliko kuzama” ndugu zetu hawa wamezama vyema katika shimo la kufunika wimbo wao, maana katika uwazi jamii ya sasa imeamka kifikra katika neno #TuzungumzeMuziki

Hivyo katika upana wa biashara ya muziki hakukuwa na sababu yoyote ya msingi ya kufanya ya hovyo ili watoe wimbo, bali mikakati yenye maana katika utoaji wa wimbo tu.

Lakini daima “Huwezi kuona msitu ukiwa msituni” Tafakari.
#TuzungumzeMuziki