‘Refa anapendelea ukiongea unapewa kadi imradi usiwaze unyonyaji’ Nash Mc

‘Refa anapendelea ukiongea unapewa kadi imradi usiwaze unyonyaji’ Nash Mc

Maalim Nash huyu ni mmoja kati ya wasanii bora wa hiphop ambaye katika vilinge vya wapenzi wa muziki wa hiphop humuita mfalme.

Tungo zenye kubeba uhalisia wa maisha ndio tungo zinazofanya mitaa impe heshima zaidi kuliko wasanii wengine wenye kusifu vyema vitu vya kipuuzi kama pombe na ngono.

Naandika,Tunazindua Mitaa, Kaka Suma, Zima, Mwanangu, ni moja kati ya nyimbo zake ambazo zimebeba uhalisia wa maisha ndani ya muziki hata nje ya muziki.

Katika wimbo wa Tunazindua mitaa ambao ni wimbo aliyomshrikisha P the mc, One Incredible, na Stereo. Hakika hii moja kati ya nyimbo bora za hiphop ambazo zimewahi kutoka katika ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Hoja ya refa anapendelea ni hoja ambayo inagusa uhalisia wa media zetu zinavyofanya juu ya wasanii wetu, upendeleo upo kwa kiasi kikubwa tena unazidi kukua kila iitwapo leo.

Na mara tu msanii akionekana akizungumzia juu ya upendeleo huo basi kifuatacho ni msanii husika kuzimwa kabisa kuchezwa kwa nyimbo zake, lakini kuzimwa kwa msanii mmoja wengine hubaki na hofu katika mioyo yao na unyonyaji huendelea na kumnufaisha zaidi mtu mmoja ambae ni mdau.

Hali hii imemgusa Nash Mc katika upande wa muziki wake, leo hii ni ngumu kusikia wimbo wa Nash Mc katika vituo vya radio au kuona kwenye vituo vya runinga.

Yote hii imetoka na misimamo yake ya kutambua haki zake na jinsi mdau anavyopendelea wasanii kadhaa lakini swala la umkoa (Ukanda) kupewa kipaumbele kwa sasa.

Leo kama wasanii wetu wangekuwa na misimamo ya Nash Mc hakika tungeweza kuwa na usawa katika mambo mengi nje ya sanaa na ndani ya sanaa katika mlengo wa usawa.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez