RAY KIGOSI TUSIWAPOTEZE WATANZANIA KWA VIJISENTI VIDOGO TUNAVYOPEWA

Vincent-Kigosi-c4t
Wakati vuguvugu la uchaguzi likiendelea kushika kasi siku hadi siku.Na wasanii wengi kutoka katika tasnia mbalimbali wamekuwa mstari wa mbele wakiposti katika mitandao ya kijamii kuhusu wagombea wa uraisi kutoka katika vyama tofauti na zaidi ni Ccm na chadema.
Ray Kigosi ni moja kati ya wasanii walioposti mtazamo tofauti juu ya baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Movie kuonesha msimamo wao katika kuwaunga mkono wagombea flani wa Urais. Msanii Ray Kigosi aliandika kwenye mtandao wa instagram.

“Usiku wa jana nimetafakari vitu vingi sana kuhusu Nchi yangu iliyobarikiwa kila aina ya utajiri wa madini mbuga za wanyama wakiwemo aina mbalimbali za wanyama wa kuvutia na hekta kubwa za misitu.Ila ninaona vipofu wengi sana wasiolewa nini tulichobarikiwa ndani ya Tanzania yetu. tumeingizwa mikenge mingi sana katika mikataba tena mibovu bajeti kandamizi Kwa watu wa hali ya chini mifumuko ya bei kila kukicha hali ngumu kwa wasanii wa Tanzania kila siku ahadi zisizotekelekeza why nasema hivyo wasanii wenzangu? tumeumia kwa kipindi kirefu sana bila msaada wowote hatuna haki miliki wa kazi zetu,zinaibiwa kama njugu sokoni kariakoo yani tulitupwa kama taka taka kwenye dampo lakini sasa hivi kipindi cha uchaguzi ndio tunaonekana umuhimu wetu tuamke kuwaambia wananchi wachague viongozi makini watakaoweza kutuvusha Watanzania kwenda hatua nyingine.
Tuna watu wengi sana nyuma yetu wanaotuamini sisi wasanii kama kioo cha jamii tusiwapoteze Watanzania kuwaambia Viongozi wa chama flani ndio wanafaa kwa vijisenti vidogo tunavyopewa. Watanzania huu ni wakati sahihi wakutulia na kuwachagua viongozi makini wanaofaa Ni katika kukumbushana tu waswahili wanasemaje utakaokatanao kuni ndio utakaota nao moto.”
Unaweza kuwa rafiki yetu faceboo.com/tizniz

instagram.com/tizneez

twitter.com/teamtizneez