RAMA DEE SINA HOFU YA MUZIKI

1350873579_RAMA_DEE___

Chini ya uvungu wa moyo wangu ni album  yake ya kwanza kabla ya kufuatiwa na album ya The Best of Rama Dee. Rama ni ni msanii wa rnb aliyewahi kufanya vyema na nyimbo kama, Kikao cha family, Sara, Kama huwezi, Make up, Najua, Kuwa na subira,Usihofie wachaga, Siowaoji na nyingine nyingi.

Rama dee hakusita kuweka wazi mtazamo wa walio wengi kutoa nyimbo kila baada ya muda mfupi, Rama Dee alisema “Mimi sina hofu katika muziki, na niko tofauti katika ufanyaji wa muziki, unajua kila mtu ana staili yake. Hivyo wanaotoa nyimbo kila baada ya muda mfupi waache watoe ila mimi sina hofu, nina staili zangu kivingine.”

Hata hivyo Rama Dee aliendelea kusema “Mimi napenda kukaa karibu na wasanii wa hiphop maana kuna heshima zaidi, waimbaji wengi wanajiongeza zaidi.”

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez