Rama Dee Aweka wazi kuhusu Lady Jaydee

Rama Dee ni moja kati ya wasanii bora wa Rnb ambao tumebahatika kuwa nao katika ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Rama dee ambaye mpaka sasa anamiliki Album mbili ambayo ya kwanza ni Chini ya Uvungu wa moyo wangu na ya pili ni The Best Of Rama Dee. Licha ya kuwa bora katika muziki wa Rnb lakini ni msanii ambaye si rahisi kusikia/kuona nyimbo zake katika vituo vya radio na runinga hapa nchini isipokuwa mtaani zaidi.

Lakini katika yote hayo amebaki kuwa bora katika muziki huo na katika vilinge vya wapenda muziki mzuri hawasiti kumuita yeye ni mfalme wa Rnb hapa Tanzania baada ya Mr Paul.

Team tizneez tumefanyanae mahojiano ambapo amezungumzia mambo kadhaa kama, Video ya kipenda roho, kufanya kazi na Jux, Ben Paul, na Belle 9, pia kuhusu Clouds Fm. Pia swala la ukaribu wake na Lady Jaydeea ambapo ameelezea kwa undani zaidi. Karibu kusikiliza hapa chini.

Batro akizungumza na Rama Dee.