Rama Dee atupiana maneno na Peen Lawyer juu ya Weusi

Rama Dee atupiana maneno na Peen Lawyer juu ya Weusi

Jina la Peen Lawyer huenda likawa geni katika masikio ya wengi sasa, ila moja kati ya watu wachache ambao walishiriki vyema katika kuweka mambo sawa kwenye muziki wa kizazi kipya mwaka 2010.

Peen Lawyer maarufu kama Kinegax ambaye ndio aliyekuwa kinara wa kusambaza Mixtape ya Ant Virus kuanzia vm 1 mpaka II ambaye sasa anaishi nchini Ujerumani.

Kupitia mtandao wa Twitter Peen Lawyer aliandika maoni yake juu ya kauli ya Young Killer ambapo hakua jambo gumu kwa Rama Dee kujibu hoja hizo.

Peen Lawyer ameandika

Lakini pia Rama Dee ambaye ni msanii wa Rnb ambaye pia alishiiki vyema katika harakati za Ant Virus hakusita kuandika katika mtandao wa picha Instagram ambapo ameandka

Kuna mtu anaitwa @kinegax huyu jamaa nafikiri haujawahi kumfahamu ila unaweza kumfahamu kupitia hapa, huyu dogo aliwah kushiriki kwenye Antivirus mixtape na alifanya kazi kubwa sana ya kuwahabarisha baadhi ya habari!

Ila kiukweli ile mixtape tuliifanya sio kwa kuchukia wasanii bali kuchukia mfumo mzima amabo ulikuwa upo kihuni kipindi kile! So nikiona leo hii wasanii au Msanii anafanikiwa kwenye Biashara yake ya muziki alafu wewe ambae ulisimama kutetea ili wafanikiwe unatokwa mapovu nakuona ni mpofu wa akili, pia ni Mtu hatari sana kwa Maendeleo ya watu!

I’m tired kwa kweli….alafu peen unatakiwa kuelewa sisi ni watoto ambao tumekulia kwenye maisha magumu sana, so nikiona unacheza na maisha ya watu haswa wasanii naona wewe ni Virus big time! :
:
Naaandika hivi kwa sababu nimekaa kimya kwa muda wa miaka zaidi ya 3 Najaribu kumuelewesha na kumkumbusha Mtazamo wa ile Mixtape na jinsi ilivyo saidia Wasanii, lakini haelewi!
:
:
Hauwezi kulazimisha kufahamika kupitia muziki Kama sio talented na hii kitu, :
:
Mimi ni mwanamuziki naheshimu kile afanyanyacho mwanamuziki mwenzagu Kama kipo kwenye uwanja wa kazi!

Alafu unatakiwa kuelewa Dunia ya leo jaribu kuongeza marafiki sio kupunguza Marafikia Mate!

Ulikaribishwa sehemu ya watu wenye akili sio wajinga so acha kutumia njia ya ile movement kwenye mambo ya kipuuzi kuchukia watu!

Fanya kazi weka juu….Kama unataka mambo ya siasa na unaipenda sana Nchi yako Ichambue Ccm ukiwa Tanzania sio upo Ujerumani unaongea vibaya kuhusu Tanzania that’s stupid! :
:
I’m out sihitaji watu Kama wewe…endelea na issue zako, alafu kumbuka watu wote unao wafahamu ni machizi wangu for real! Bye bye!

 

 

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment