Rama Dee Aeleza sababu za kuweka Rnb kwenye Singeli.

IMG_5824-660x330

Rama Dee Aeleza sababu za kuweka Rnb kwenye Singeli.

Kipenda roho ni wimbo wake ulifanya vyema kwenye ramani ya Rnb Tanzania. Rama Dee ambaye anashikilia album mbili mpaka sasa ambayo ni Chini ya uvungu wa moyo wangu na ya pili ni The best of Rama Dee.

Mapema leo hakusita kuweka wazi kwanini ameamua kuweka Rnb katika muziki wa singeli. Ambapo Rama Dee amesema “Kwanza ni kutoa tafsiri ya singeli ni muziki wa uhuni kama wengi wao wanavyodhani. Na kupitia mimi wajue kuwa muziki huu ni kazi kama kazi nyingine, hata mzazi akisikia mwanae anafanya singeli asiwe na shaka”

Mazoea ni wimbo wake wa singeli ambao amefanya na msanii wa singeli anaeitwa Yuda ambaye inaaminika kuwa ni msanii pekee wa kike anaeimba singeli.

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez