PROF JAY AZUNGUMZIA TAMASHA LA DEMOCRACY IN DAR

IMG_1829

Moja kati ya wasanii wa  walioamua kuingia kwenye siasa ni Joseph Haule a.k.a Prof Jay ambaye ameamua kugombea ubunge katika jimbo la Mikumi Morogoro kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA.

Leo mapema katika hotel ya Kebby Hotel iliyopo Bamaga Dar es salaam,Prof jay alitoa yake ya moyoni kuhusu tamasha la Democracy in dar,ambapo Prof jay alisema ”Ni kitu kizuri kwa sisi wasanii kujitoa kutoa elimu juu ya uchaguzi unaokuja hivi karibuni.Unajua wasanii tuna nguvu katika swala zima la uhamasishaji hivyo naomba wasanii wengine tusimamie zaidi katika hili tamasha,Na pia tusiangalie itikidadi za vyama watu wote wanaweza kuja  na tukafanya kazi moja ya kuelimisha huku tukitoa burudani kwa wakati mmoja.

KALA JEREMIAH MUDA UMEFIKA TUFANYE MAAMUZI SAHIHI

IMG_1852

Kala Jeremiaha ni miongoni mwa wasanii ambapo walikuwepo katika mkutano na waandishi wa habari,katika hotel Kebbys Hotel.

Kala alisema”Vijana wenzangu muda umefika wa kuchagua viongozi shupavu wenye uchungu na taifa hili,sasa vile vitambulisho tutumie kwenye kupiga kura tuache ule usela wa flani jembe huku tumekaa maskani.Kwaiyo mje kwa wingi kwenye tamasha la Democracy in dar ili tupeane elimu ya kutosha.

JUMA NATURE WATU WANGU HATUNA MUDA WA KUPOTEZA

IMG_1840

Msanii aliyekuwa kivutio katika mkutano na waandishi wa habari alikuwa na Juma Nature,ambaye alionekana akiwa katika hali ya kuchangamka na kuongea maneno ya utani na kufanya waandishi kutabasamu muda wote.

Juma Nature alisema”Mimi sina mengi mana wenzangu walishanongea mengi ila kikubwa watu wangu hatuna muda wa kupoteza kikubwa ni kutokea pale katika viwanja vya Zakhem Mbagara tuongee mengi.Mimi kwangu ni kitu kikubwa nawaomba vijana wenzangu mjitokeze kwa wingi.

MSAGA SUMU MENGI MAZURI YATATOKEA ”DEMOCRACY IN DAR”

IMG_1857

Msaga sumu ni miongoni ya msanii atakeyekuwepo katika tamasha la Democracy in dar.Msaga Sumu hakuwa na maneno mengi zaidi ila alisema”mengi mazuri yatatokea  kwenye tamasha hili cha msingi watu waje kwa wingi.

Tamasha hili linatarajiwa kufanyika katika viwanja ya Mbagara Zakhem tarehe 16/8/2015 kuanzia saa 7 mchana mpaka sa 12 jioni.Hata hivyo litahusisha wasanii wengi kama,Ney wa mitego,Kala Jeremiah,Roma Mkatoliki,Mkoloni pamoja na Mh wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi.Lakini pia wasanii wa bongo muvi watakuwepo kama,aji Adam aka Baba Haji, Jacqline Wolper,Auntie Ezekiel,Shamsa Ford,na Jimmy Mafufu Pia na watu wengi maarufu.

Mwisho.

unaweza kuwa rafiki yetu facebook.com/tizniz

twitter.com/team tizneez

instagram.com/tizneez