Prof Jay Aweka wazi msimamo wake juu ya kutumbuiza wimbo wa CCM na CUF na Juma Nature.

Prof Jay Aweka wazi msimamo wake juu ya kutumbuiza wimbo wa CCM na CUF na Juma Nature.

Prof Jay ni moja kati ya wasanii wakongwe waliochangia kukua na kuenea kwa bongo fleva/hiphop ndani ya nchi na nje pia.

Lakini pia inaamikia Prof Jay ndiye msanii ambaye anaongoza kuwa na ‘Hits songs’ nyingi zaidi.

Prof Jay ambaye jina lake kamili ni Joseph Haule lakini kwasasa ni Mh Mbunge wa Jimbo la Mikumi liliopo katika Mkoa wa Morogoro. Nafasi hiyo ya Ubunge ameipata kupitia tiketi ya Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa.

Ila katika historia ya muziki wake amewahi kutunga tungo nyingi zenye ujumbe tofauti tofauti.

Kupitia mtandao wa Twitter shabiki hakusita kumuuliza Mh Prof Jay, shabiki ameuliza “Mfano kuna tamasha ukasimamishwa na juma nature mkaimbe ule wimbo wa ccm na cuf utaiimba?

Ambapo Prof Jay alijibu “Why not? Mimi bado ni mwanamuziki, shughuli yeyote inayohusu muziki naweza kufanya muda wowote/popote ili mradi niwe sijabanwa na majukumu.

Mwisho.

Attachment