PROF JAY ATANGAZWA MBUNGE WA MIKUMI

IMG_3064
Joseph Haule maarufu kama Prof Jay ambae alianza muziki wa rap miaka ya 1994 akiwa mmoja kati ya wasanii wanaunda kundi la Hard Blasterz.Ambao walifanikiwa kutoa album iliyokwenda kwa jina la funga kazi
Licha ya kuwa kati ya wasanii bora wakati wote tangu aanze kufanya muziki wa hiphop hapa nchini Tanzania,prof pia ameshapata tuzo nyingi za ndani na nje ya Nchi.
Mapema mwaka huu aliamua kujitosa katika kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Mikumi ndani ya mkoa wa Morogoro,kupitia tiketi ya chama CHADEMA chini ya mwamvuli wa Ukawa.Licha ya kampeni za mwaka huu kuonekana ni zenye ushindani lakini msanii Prof Jay ameibuka mshindi katika jimbo hilo la mikumi.
Prof Jay ameshinda kwa Kura 32259,huku akifuatiwa na Jonas NKYA (CCM) Kura 30425 kwahiyo ameshinda kwa tofauti ya 1834.Hivyo sasa ni mbunge rasmi wa Jimbo la Mikumi.
Na Prof Jay n msanii wa pili wa muziki wa rap maarufu kama hiphop kushinda nafasi ya ubunge.Msanii wa kwanza alikuwa ni rafiki yake wa Joseph Mbilinyi a.k.a MR II Sugu ambaye nae ametangazwa jana kuweza kutetea kiti chake katika jimbo la Mbeya Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA chini ya mwamvuli wa ukawa.
Team tizneez inampongeza/inawapongeza kwa ushindi huo.