PRO JAY ACHAGULIWA KAMATI YA BUNGE

IMG_3152

Mh Joseph Haule maarufu kama Prof Jay ambaye ni mbunge wa Jimbo la Mikumi linalopatikana katika  mkoa wa  Morogoro.Prof jay ambaye pia ni moja kati ya wasanii wachache walichonga njia ya muziki wa bongo fleva/hiphop mpaka hapa ulipofika.

Katika uchaguzi mkuu 2015 ambao ulihusisha ngazi ya Udiwani,Ubunge na Urais, Prof jay alichaguliwa na wananchi wa Mikumi kuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia tiketi ya Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa.

Na mapema mwaka huu 2016 Mh Joseph Haule amechaguliwa katika kamati ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC). Na katika kamati hii ameungana na wabunge wenzake ambao ni Mh.Esther Nicholas Matiko,MH. Sebreena Hamza Sungura, Mh. Joseph George Kakunda pamoja na Mh.Fatma Hassan Toufiq.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Instagarm tizneez

Facebook tizneez