PANCHO LATINO NA JABIR SALEH WAZUNGUMZIA KIFO CHA LUCKY STAR

images
Lucky Star ni miongoni mwa washiriki waliowahi kushirki katika shindano la The jump Off Michano 2015 lilioendeshwa na Times Fm radio hapa Jijini Dar es salaam.Shindano hilo lilisimamiwa na mtangazaji wa kipindi husika cha The jump off ambaye ni Jabir saleh.Shidano hilo la rap music lilihusisha vijana takribani 400 lakini waliobahatika kushiriki katika fainali zilizofanyika katika ukumbi wa Dra live ni vijana 10 tu.Na miongoni mwa hao 10 ni pamoja na marehemu Lucky Star amabye ndiye mshiriki aliyekuwa na umri mdogo kuliko wote.Lakini kutokana na siku ya fainali kutokuwa na hali nzuri kiafya hakuweza kufanya vizuri lakini alibahatika kuingia katika 5 bora,Licha ya kuishia katia mchujo huo wa 5 bora na kushindwa kuendelea kuingia katika 3 bora.Ila kwa uwezo alionyesha tangu siku ya kwanza wa shindano hilo ulimvutia Producer Pancho Latino na kumpa nafasi katika studio za Bhitz Recods.Pancho akizungumza leo baada tu ya kupata taarifa hizo alisema”nimesikitishwa na taarifa hizi za kufariki kwa Lucky Star,mara ya kwanza nilimuona kwenye mashindano na baadae nilimuambia aje studio na alifika tu.Kikubwa nilimwambia afanye mazoezi kuna baadhi ya vitu vidogo tu akae sawa ili turekodi,Hata jana tumewasiliana na mipango ilikuwa mizuri lakini ndio hivyo kifo kimemkuta sina kingine zaidi ya kuwapa pole wote walioguswa na msiba huu wa Lucky Star.”
Pia Jabir Saleh ambaye ni miongoni mwa watu walioguswa na msiba huo alisema”nimepokea kwa masikitiko makubwa jioni hii taarifa kuwa mmoja kati ya vijana walioingia kumi bora ya mashindano ya #thejumpoffmichano2015 aitwae Lucky starr amefariki dunia leo baada ya kuugua ghafla.majira ya asubuhi leo hii.Na msiba utakua kesho pale mbagala. Inna lillahi wainna ilaihi rajiuun!
Team tizneez inatoa pole kwa wote walioguswa na msiba huu.
picha chini Lucky Star enzi za uhai wake akiwa katika mashindano ya the jump off michano
Capture