PAH ONE HATUKUWA NA CHAGUO ZAIDI YA CHRISTIAN BELLA

IMG_3515
Pah One ni miongozi mwa makundi ya bongo fleva yaliyowahi kufanya vizuri kabla ya kutengena miaka kadhaa iliyopita.Pah one ilikuwa inaundwa na Aika, Nahreel, Oral na Igwe,lakini sasa inaundwa na Oral na Igwe wakati Nahreel na Aika wanaundwa kundi la Navykenzo.
Akiongea na Team tizneez moja kati ya mwanachama wa Pah One,Oral alisema”ni muda mrefu tumekuwa kimya lakini tumeshafanya ngoma za kutosha,lakini wimbo tulioamua kurudi nao ni Magoma tuliomshirikisha Christian Bella.
Wakati tunatafakari kazi hii hatukuwa na chaguo zaidi ya Christian Bella,sababu jamaa anafanya vizuri na sio leo wala jana siku zote Bella amekuwa msanii mzuri, pia na aina ya ngoma tuliyotaka ilihitaji tu awepo Bella
Watu wajiandae na ngoma yetu ya Magoma ambayo amesimama Bella na imetengenezwa na Imma the boy,tutaachia audio na video kwa pamoja maana tayari video tumeshafanya kwa director Minz Mims.
IMG_3689
IMG_3644

Unaweza kuwa rafiki yetu facebook.com/tizniz

instagram.com/tizneez

twitter.com/tizneez