Onyesho la kinasa lawakutanisha wanasanaa wa Dar es salaam na Morogoro

Onyesho la kinasa lawakutanisha wanasanaa wa Dar es salaam na Morogoro

Kinasa ni moja kati ya matumbuizo makubwa ya wazi ambayo yamekuwa yakiendelea kufanyika katika Jiji la Dar es salaam. Tumbuizo hili la Kinasa hufanyika katika wilaya ya Temeke katika viwanja vya shule ya msingi Madenge

Kinasa kwa maana pana ni Kiswahili Na Sanaa. Uhalisia wa jukwaa hili la Kinasa ni katika kuinua Sanaa zote ambazo zitasaidia kuendelea kukuza na kueneza Kiswahili na wakati huo huo kuonyesha ukubwa wa lugha ya Kiswahili katika upana wa Sanaa zote.

Jukwaa hili halichagui aina ya Sanaa kama wengi wanavyodhani, jukwaa hili ni jukwaa huru kwa Sanaa za aina zote, kuanzia kuimba, ushairi, uchoraji, na Sanaa nyinginezo.

Licha ya walio wengi kudhani kuwa jukwaa hili la Kinasa ni maalum kwaajili ya watu wa hiphop. Nash Mc hakusita kuweka wazi jambo hili ambapo aliiambia Team Tizneez “Jukwaa hili la Kinasa ni la kila mtu anaefanya Sanaa zote, hapa hatuchagui mtu. Na mialiko tunatoa kwa wasanii wote bila kujali nani ni nani licha ya wenzetu ambao wanaofanya Sanaa nyingine kushindwa kutokea. Ila hatutaacha kuwahimiza umuhimu wa jukwaa hili.

Jukwaa la Kinasa limefanyika  kwa mara ya mwisho tareh 27/11/2016 ambapo limebahatika kupata ugeni mkubwa kutoka Morogoro, ugeni wa Mwandishi wa vitabu Ndugu Majid Mswahili, pia ugeni wa MH mbunge Abdallah Mtolea wa Jimbo la Temeke. Ambapo Mh Mbunge hakusita kutoa pongezi kwa waandaaji wa Jukwaa la Kinasa, lakini hakusita kutoa ahadi za kusaidia zaidi jukwaa hilo akiweka wazi juu ya mchango wa kuwapatia jukwaa kubwa la kutumbuiza na mambo mengine.

Lakini pia vijana toka Morogoro ambao wanajulikana kama Moro Youth Talent, kupitia msemaji wao alisema”Tumefurahishwa mno na ujio wa watu wengi ambao wamejitokeza hapa, lakini pia na sisi tunawakaribisha nyumbani Morogoro. Majukwaa kama haya yanatujenga kisanaa lakini pia kutujenga katika hali ya umoja, pia hata kutuunganisha kisanaa, hivyo kuna kila sababu ya Serikali na wadau kutoa ushirikiano katika mambo haya mazuri. Nichukue nafasi hii kumpongeza Nash Mc na Team yake kwa kuandaa jambo hili”.

Jukwaa hili la Kinasa litafanyika tena mwakani 2017 hivyo endelea kuwa karibu na www.tizneez.com ili kujua zaidi kile ambacho kitajiri.

Tazama picha chini matukio ya jukwaa la kinasa.

 

IMG_3080

Picha ya muonekano wa nemba ya Kinasa.

 

IMG_3084

Picha Nash Mc akiongea jambo na watu waliojitokeza kwenye tumbuizo hilo.

IMG_3097

 

Picha mashabiki wakichukua picha kwa kumbukumbu na wengine wakifutilia kwa umakini
IMG_3101 IMG_3104 IMG_3107 IMG_3109 IMG_3113

 

Picha Nash Mc akiwa na mwandishi wa Vitabu Ndugu Majid Mswahili (Upande wa kulia)IMG_3137 IMG_3145

 

Msanii wa hiphop Bassalt akionyesha uwezo wake mbele ya mashabiki wa jukwaa la KinasaIMG_3172

 

IMG_3300 IMG_3301

Nash akiwatambulisha Moro Youth talent kutoka mkoani Morogoro

IMG_3324 IMG_3329 IMG_3334 IMG_3165 IMG_3189 IMG_3209 IMG_3301 IMG_3343