“Ommy G amekosea tu kusema mimi nimefariki” Dullayo.

“Ommy G amekosea tu kusema mimi nimefariki” Dullayo.

Bila yule ni wimbo wake ambao ulitambulisha vyema kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Ambapo wimbo alimshirikisha Mwana Fa huku ukitengenezwa na Marko Chal ndani ya Mj Records.

Naumia roho, Twende na mimi, ni miongoni mwa nyimbo zake ambazo pia zimeweza kufanya vyema zaidi.

Mapema leo msanii Ommy G alikuwa akituma ujumbe ambao unasema “Baba Dullayo amefariki”.

Ambapo mapokeo ya watu ni yakuwa “Dullayo amefariki”.

Dullayo ameweka wazi yakuwa “Baba yangu mzazi ndiye amefariki, lakini naona Ommy G amekosea tu katika kufikisha taarifa hizo kwa watu.

Mimi nipo na afya njema tu, lakini nimempoteza Baba yangu. Na sasa tupo tunaendelea na mipango ya mazishi hapa nyumbani Ukonga”

Team Tizneez tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu.

Na daima “Kifo na kiumbe, kiumbe na kifo” Na Upumzika kwa Amani Mzee Dullayo.