NYIMBO 10 ZILIZOFANYA VIZURI 2015 BONGO FLEVA/HIPHOP

analogdigital_03

Bongo fleva/hiphop ni mziki ulioanza miaka ya 1990,ila mwaka 2015 kumekuwa na vipaji vingi vilivyoibuka na pia baadhi ya wasanii wakongwe kuendelea kufanya vyema.

Team tizneez inakuletea nyimbo 10 zilifanya vizuri mwaka 2015, Hii ni kwa mujibu wa tizneez.com. Kuna nyingi zilizofanya vizuri ila hapa tumetazama zile zilizofanya zaidi.

Hizi ni baadhi ya nyimbo 10 zilizofanya vizuri 2015

Shikorobo,Hii ni ngoma ya mkali Shetta aliyofanya na Kcee tokea Nigeria,wimbo huu ulifanya vizuri kuanzia audio na hata video na kufanikiwa kushika chat mbalimbali za nje na ndani ya Tanzania.

Shauri zao,Huu ni wimbo halali wa Belle 9 tokea pande za Morogoro ambaye sasa pia alipata bahati ya wimbo wake kuchezwa katika vituo vikubwa vya Tv kama trace.2015 ulikuwa mwaka mzuri zaidi kwa Belle maana alipata nafasi ya kuwa balozi wa kampuni moja kwaajili ya matangazo.

Nana,ni wimbo mkubwa uliweza kupenya kila mahala na kushika chat mbalimbali katika Africa na kuzidi kumpa heshima Diamond Platnumz, wimbo huu alimshirikisha msanii tokea Nigeria Mr flavour

Chekecha Cheketua,Hupenda kujiita King Kiba,ambaye ameendelea kufanya poa tangu arudi na wimbo wake wa mwana dar es salaam.Hata hivyo licha kuwepo kwa wimbi la kufanya kolabo nyingi za wasanii wa Tanzania na Nigeria Ally kiba ameendelea kufanya kazi yeye kama yeye.

Nashindwa,Huu ulikuwa wimbo mkubwa 2015 kutoka kwa king of melody Christian Bella,Ambaye pia ni kiongozi wa kundi la Malaika band yenye maskani yake Dar es salaam.

Nivumilie,Baraka da prince ambaye mwaka 2015 alishinda tuzo ya KTMA kama msanii chipukizi na akaendelea kuthibitisha ukubwa wake baada ya kutoa nivumile na Ruby na kufanya vizuri pia.

Nusu Nusu,Hii ni ngoma ya mkali Joh Makin iliyofanya wengi kustuka na ile video yake.Huu ni wimbo uliofanya vizuri pia katika mwaka 2015.

Zigo,Mkali Ay ambaye amekuwa ni mtu wa vitendo zaidi kuliko maneno hapa alidhihirisha ukubwa wake katika ame hii pale ambapo aliachia ngoma ya zigo na kutawala kwenye vichwa vya wapenda muziki wa bongo fleva.

Game,huu ni wimbo ulifanya pia 2015,wimbo huu ni mali ya Navy Kenzo walimshirikisha Vanessa Mdee,ambapo wimbo huu ulifanya vizuri nje na na ndani ya mipaka ya Tanzania.

No body but me,Huu ni wimbo wa mwisho uliofanya vizuri mwaka 2015,Mkali Vanessa Mdee hapa katika wimbo huu alifanya na mkali toka south africa KO.

Hizi ni nyimbo zetu 10 zilizofanya vizuri 2015,unaweza kututumia maoni yako kupitia Teamtizneez@gmail.com au

cc# www.tizneez.com

instagram@tizneez

twitter@tizneez

facebook@tizneez