Nini kimewapoteza wasanii hawa wawili wa muziki wa kizazi kipya?

artists-recording-artists-large-icon

Nini kimewapoteza wasanii hawa wawili wa muziki wa kizazi kipya?

Muziki wa kizazi kipya umekuwa rahisi zaidi kuliko ambavyo ilikuwa miaka ya nyuma. Ni wazi muziki huu umekuwa rahisi tofauti na zamani hasa katika swala zima la uandishi pia katika nafasi ya vyombo vya habari.

Leo Team Tizneez imetizama katika upande wa bongo hiphop. Kuna wasanii wengi wa muziki huu wa hiphop hapa nchini Tanzania.

Lakini wapo wasanii ambao uwezo wao ulikuwa ni wa kiwango cha juu, lakini katika uhalisia hawajawahi kufanya vyema zaidi katika vyombo vya habari. Ila ni wasanii ambao wanaheshima kubwa katika majukwaa mengi ya hiphop.

Pig Black, ni moja kati ya wasanii wakali ambao tumebahatika kuwa nao katika muziki wa hiphop hapa Tanzania. Lakini ni wazi ukimya wake umekuwa ni wa muda mrefu ambao wengi wao hawajui kwanini imekuwa ni kimya kiasi hicho.Mara nyingi tumekuwa tukiskia sauti yake katika nyimbo ambazo hushirikiana kundi la B.O.B na Micharazo. Pig Black ni msanii na flow nzuri,na uandishi pia, lakini ni hatujui ni kwanini ukimya wake umekuwa ni wa muda mrefu. Nini mnataka ni wimbo wake uliofungua njia yake katika muziki wa kizazi kipya ambao mpaka sasa ni wimbo mmoja wapo katika nyimbo bora za hiphop.

Jose mtambo, huyu ni msanii ambaye yupo chini ya Tongwe Records na ameshatoa nyimbo nyingi kali. Pia ni mmoja kati ya wasanii ambao waliwahi kushiriki katika shindano la mfalme wa Rhymes ambao alishinda Afande Sele mwaka 2004. Jose Mtambo ambaye msanii pendwa pande za Kigamboni, “sio busara” ni moja kati ya nyimbo zake ambazo zimekuwa zikiamsha hisia za walio wengi katika kumbi mbalimbali mara tu inapokuwa inachezwa. Hakika ni moja kati ya wasanii wa bora wa hiphop katika tuzo za mtaani sio zile zenye kupangwa apewe nani

Hawa ni baadhi ya wasanii wa hiphop ambao Team tizneez inajua na kuheshimu ukubwa wa vipaji vyao.

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez