NIKKI WA PILI “NIONAVYO SIASA HIZI”

IMG_6967

Nikki wa Pili ni msanii wa rap kutoka kampuni ya Weusi inayoundwa na wakali kama,Joh Makini,Bonta,Gnako na Lord Eyez.

Katika kipindi cha kusubiri matokeo ya uchaguzi mkuu ambao ulijumuisha ngazi zote ikiwa ni Udiwani,Ubunge na Urais,wasanii mbalimbali wamekuwa wakiendelea kutoa mitazamo yao.Kupitia mtandao wa picha msanii Nikki wa Pili aliandika”Nionavyo siasa hiz 1.Ukanda wa kaskazini na ukanda wa ziwa. 2.Trendi inaonesha 40% watakuwa hawajapiga kura .3 Mjini na Vijijini naona posta kibao za magroup watu wakikebehi watu wa vijijini,bado watu hao hao wanasema uchaguzi  sio huru na haki,ila hajioni yeye akiingilia uhuru na haki yao hao anao wakebehi. 4.Wengi walioshindwa pinzani ama tawala wamelaumu usimamizi na mahesabu kiufupi kila mtu anataka madaraka. 5.Uchaguzi umezingatia sana uchama sio harakati cc Kafulila .6. Uhuru na haki una mashaka Zanzibar wamethibitisha hilo. 7.Naona mpaka jinsia zina laumiana eti wanaume vs wanawake. Hitimisho mshindi anasema asante mungu, mshindwa mungu atawahukumu.

Nami natenda kama baba yangu aliyejuu,wote atakaye shinda ama kusindwa nawapa amani ya moyo acha niendelee na issue zangu”

Team tizneez inapenda kusisitiza amani katika kipindi hiki Mungu ibariki  Tanzanianininaona