NIKKI WA PILI NI RAHISI MSANII MPYA KUFANYA VIZURI

index
Good boy ni wimbo uliomtambulisha kwenye ramani ya muziki wa bongo fleva nchini Tanzania.Wimbo huo wa good boy alimshirikisha mkali Rama Dee ambaye ameonekana kuwa ni moja kati ya mkali wa RNB kati ya walio wengi.
Nikki wa Pili akitambulisha wimbo wake mpya wa Baba Swalehe katika kipindi cha The Jump Off kinachotangazwa na Jabir Saleh ndani ya Times Fm radio Nikki alisema “kwangu naona ni rahisi manii mpya kufanya vizuri kuliko msanii aliyekuwa kwenye game kwa miaka mingi.Unaona kama Chemecal vile unajua ukishakuwa kwenye game kwa miaka mingi kuna ugumu maana watu wanakuwa wamekuzoe.Hivyo inabidi ukaze zaidi ila ni rahisi zaidi kwa msanii mchanga.Hata hivyo Nikki aliwaasa wasanii wenzake ambao sasa wanaachia tu nyimbo katika social media na kuwataka wapeleke radio maana watanzania walio wengi hawana uwezo wa kupakua nyimbo hizo kwa changamoto nyingi,ikiwemo mtandao.Lakini radio inafika mahali pakubwa zaidi.