Nikki wa Pili Ahoji juu ya kukamatwa wa Nay wa Mitego


Nikki wa Pili Ahoji juu ya kukamatwa kwa Nay wa Mitego

Sweet Mangi ni moja kati ya nyimbo zake Nikki wa Pili ambazo zimewahi kufanya vyema kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya ndani ya nchi na nje pia

Nikki wa Pili ambaye ni miongoni mwa marapa waliopo katika mwamvuli wa hiphop amekuwa na uthubutu wa kutoa hoja nyingi katika maswala ambayo yanaendelea ndani ya muziki na hata nje ya muziki.

Mapema leo kumekuwa na taarifa za kukamatwa na kushikiliwa na polisi kwa msanii wa Bongo Fleva Nay wa Mitego. Na taarifa hizo zilitoka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa picha Instagram. Ambapo Nay ameandika “Nimekamatwa kweli. Muda Huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza Kazi yangu iliyo ni leta. Napelekwa Mvomelo Police. Nawapenda Watanzania wote.✊🏿✊🏿 #Truth #Wapo”

Baada ya taarifa hiyo kuzagaa hasa kwenye mitandao ya kijamii,msanii Nikki wa Pili hakusita kuweka hoja zake katika mtandao huo wa picha ‘Instagram’ambapo ameandika “Sijui kwanin kakamatwa ila kama ni swala la wimbo bora shauri lifanyiwe kazi na basata na sio police kama ilivyokuwa kwa nyimbo zingine namaanisha kama atakuwa amekamatwa kwa sababu ya wimbo, ila mim sio mjuzi wa sheria labda alberto msando atusaidie….#free nay”

Mwisho

Tupe maoni yako hapa chini

Shabiki una mtazamo gani juu ya haya yanayoendelea?