Nikki Mbishi, Wakazi, P The Mc, na Songa ndiyo chaguo la watanzania waishio Marekani.

Nikki Mbishi, Wakazi, P The Mc, na Songa ndiyo chaguo la watanzania waishio Marekani.

Wengi wamekuwa na maswali mengi juu ya vipande vifupi vya video viliyosambaa kwa haraka leo kwenye mtandao wa picha ‘Instagram’.

Na vipande hivyo vya video vimemuhusisha zaidi Nikki Mbishi, Songa, Wakazi, na P The Mc.

Vipande vile vya video ni wimbo ambao watanzania waishio Marekani (Diaspora) wametaka wasanii hao washiriki katika kuutengeneza wimbo ambao una maudhui ya siku yao #TanzaniaDay2018.

Na siku hiyo huazimishwa kila mnamo mwa tarehe 26/4.

Na mwaka huu imekuwa tofauti katika kuwashirikisha wasanii ili siku hiyo iweze kufana vyema.

Na wasanii shiriki ni Nikki Mbishi, Wakazi, P The Mc na Songa, wakati muongozaji video akiwa ni Mekcy Kaloka (Ngome Video) na audio imefanyika kwenye studio za City Ocean chini ya Black Beatz.

#TuzungumzeMuziki #TanzaniaDay2018.