Nikki Mbishi awaandikia ujumbe Wasafi Tv baada ya kucheza wimbo wake

Nikki Mbishi awaandikia ujumbe Wasafi Tv baada ya kucheza wimbo wake.

Kupitia mtandao wa picha ‘Instagram’ Nikki Mbishi ameweka ujumbe wake mara baada ya wimbo wake wa Nimekumis kucheza na kituo cha Runinga Wasafi.

Ambapo Nikki Mbishi ameandika
“Asante #WASAFITV nyie mmecheza wimbo wangu #NIMEKUMISS bila hata mimi kuwaletea.

Najua ndio mnaanza ila msisahau kuendelea hivi hivi.

Hakuna kitu kinachojenga na kuimarisha misingi ya sanaa kama ushindani wenye usawa “Fair Competition”

Hii inamaanisha anayestahili na apate na asiyestahili akose japo #FITNA zipo tu.

Tumeshuhudia umwinyi na ubeberu kwa kipindi kirefu sana,wapo ambao walitaka uMungu mtu lakini walijishtukia wakabwaga na wengine walibwagwa na hiyo ni kwa sababu ya kuleta umatabaka wa kanda fulani na kanda fulani na kujuanajuana sana kiasi kwamba akina sisi tusiofungamana nao tukaishia kutengwa na kuonekana “VINEGA”

Kila la kheri kwenye hii ligi ya mbuzi kuna siku daraja litapanda tutacheza ya ng’ombe na mpaka tembo nini simba.

Ipo siku watajihoji na kujijibu wenyewe.

Cc @wasafitv”